Sport
Dollar
43,1388
0.21 %Euro
50,2459
-0.08 %Gram Gold
6.246,2500
0.83 %Quarter Gold
10.381,6000
0.77 %Silver
110,7700
4.07 %Mabadiliko hayo ambayo yamefanyika ndani ya siku 54 tangu kutangazwa kwa Baraza la Kwanza la Mawaziri wa kipindi cha pili cha serikali ya Awamu ya Sita.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri Januari 8.
Mabadiliko hayo ambayo yamefanyika ndani ya siku 54 tangu kutangazwa kwa Baraza la Kwanza la Mawaziri la kipindi cha pili cha serikali ya Awamu ya Sita.
Paul Christian Makonda, ambae awali alikuwa Naibu Waziri wa Habari, hivi sasa amepewa Wizara kamili ya Habari, Sanaa na Utamaduni, akichukua nafasi ya Profesa Palamagamba John Aidan Kabudi, ambae sasa ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum).
Rais Samia pia, alitengua uteuzi wa Boniface George Simbachawene ambae alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, na nafasi yake kuchukuliwa na Patrobas Paschal Katambi, ambae awali alikuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.
Makonda na Katambi ni miongoni mwa mawaziri waliopanda kwa kasi ndani ya muda mfupi.
Mbali na kufanya mabadiliko katika safu yake ya mawaziri, Rais Samia pia amefanya teuzi nyengine kadhaa ikiwemo za makatibu wakuu na mabalozi.
Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Tanzania, Rais Samia alishinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kwa asilimia 97.66.
Hata hivyo, Uchaguzi huo uligubikwa na vurugu za baada ya uchaguzi kufuatia maandamano ya waliokuwa wakidai mabadiliko nchini humo.
Ingawa hakuna idadi kamili iliyotolewa, lakini kuna madai ya watu kadhaa kupoteza maisha, huku wengine kujeruhiwa.
Wakati wa kuliapisha Baraza lake la Mawaziri mwishoni mwa 2025, Rais Samia, aliweka wazi kwamba, hatochelewa kufanya mabadiliko iwapo hataridhishwa na utendaji kazi wa mtu.
Comments
No comments Yet
Comment