Sport
Dollar
0,0000
%Euro
0,0000
%Gram Gold
0,0000
%Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Somalia inaunga mkono wito wa Saudi Arabia wa kutaka majadiliano mjini Riyadh kama ‘mchakato sahihi wa kisiasa’ wa kutatua matatizo nchini Yemen, inasema idara ya Uhamiaji ya Somalia
Somalia imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya kutumiwa kwa anga yao na Aidarous Al-Zubaidi, mkuu wa kundi linalotaka kujitenga la Baraza la Mpito la Kusini (STC), idara ya uhamiaji ya Somalia ilisema siku ya Alhamisi.
Katika taarifa, Idara ya Uhamiaji na Uraia (ICA) ilisema kuwa inashirikiana pamoja na mamlaka zingine za kitaifa kuthibitisha kama anga ya Somalia na viwanja vyake vya ndege vilitumika kumsaidia “kiongozi wa kisiasa anayesakwa” ikiwa ni ukiukwaji wa sheria ya Somalia au utaratibu wa kutoa idhini.
Kama itathibitishwa, idara hiyo inasema, hii itakuwa ukiukwaji mkubwa wa uhuru wa Somalia na sheria zake za uhamiaji, ikisisitiza kuwa kumsaidia mtu anayesakwa au kufanya operesheni katika maeneo yao bila idhini “haliruhusiwi.”
Muungano wa vikosi unaoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen unadai kuwa UAE ilimuondoa kimagendo Al-Zubaidi kutoka Yemen, ukisema alisafiri hadi kwenye eneo lililojitenga la Somaliland kwa boti na baadaye kupanda ndege kupitia Mogadishu hadi Abu Dhabi.
Ukiukwaji wa makubaliano
Juhudi zozote za Al-Zubaidi “kukwepa mchakato, ikiwemo madai ya kusaidiwa na nchi za nje, zitatofautiana na zile za kidiplomasia,” aliongeza.
Ilionya kuwa iwapo itathibitika kuwa kulikuwa na ukiukwaji, itakuwa kinyume na makubaliano na ukiukwaji wa sheria ya kimataifa.
“Hatua madhubuti zitachukuliwa kulingana na matokeo ya uchunguzi kuhakikisha uwajibikaji kamili kwa ukiukwaji wowote utakaobainika,” idara hiyo ilisema.
Muungano huo unaoongozwa na Saudi Arabia mapema ulisema Al-Zubaidi alishindwa kutimiza masharti ya kusafiri kwenda Riyadh kwa mazungumzo, badala yake akakusanya vikosi kuelekea Al-Dhale kusini magharibi mwa Yemen.
Msemaji wa muungano huo Meja Jenerali Turki Al-Maliki baadaye alisema Al-Zubaidi alikimbia Aden kwa njia ya bahari kala ya kuondoa eneo hilo kwa ndege, madai yyaliyokanushwa na STC, ambao wanasema kiongozi wao bado yuko kwenye mji huo.
Wiki iliopita, Saudi Arabia ilishtumu UAE kwa kushawishi vikosi hivyo kutekeleza operesheni ya kijeshi karibu na mpaka wa nchi hiyo wa kusini eneo la Hadhramaut na Mahra. UAE inakanusha madai hayo.
Kaskazini na Kusini mwa Yemen waliungana Mei 22, 1990, na kuunda Jamhuri ya Yemen.
Comments
No comments Yet
Comment