Sport
Dollar
43,1472
0.23 %Euro
50,2891
0.04 %Gram Gold
6.201,2100
0.1 %Quarter Gold
10.336,4400
0.33 %Silver
107,8500
1.33 %Mgombea wa urais wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine, amesema kuwa iwapo atapata ridhaa wa wananchi ya kuliongoza taifa hilo, basi atapitia upya mikataba ya mafuta ya nchi hiyo.
Robert Ssentamu Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine, ambaye ni mgombea mkuu wa upinzani katika uchaguzi huo, alisema kuwa serikali yake itachunguza makubaliano yote kati ya Uganda na makampuni ya kimataifa ya mafuta, na kubadilisha yale yatakayobainika kutokuwa na manufaa kwa Waganda.
Uganda inatarajia kuanza uzalishaji wa kibiashara wa mafuta ghafi baadaye mwaka huu, pale ambapo visima vinavyoendeshwa na kampuni ya Ufaransa ya TotalEnergies, kampuni ya China ya CNOOC, pamoja na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda vitakapoanza kufanya kazi kikamilifu.
Makampuni ya TotalEnergies na CNOOC yanafanya kazi chini ya mikataba ya kugawana uzalishaji na serikali ya Uganda.
“Tutaipitia kwa makini mikataba yote,” alisema Bobi Wine, ambaye awali alikuwa mwanamuziki maarufu na sasa anapambana na Rais Yoweri Museveni kwa mara ya pili mfululizo.
Uchaguzi wa mwaka 2021 Bobi Wine alipata asilimia 35 ya kura.
Bobi Wine alizungumza hayo katika mahojiano na Shirika la Habari la Reuters mjini Kampala.
“Na sehemu yoyote ya mikataba hiyo ambayo haitawanufaisha Waganda, bila shaka itarekebishwa.”
Waziri wa habari wa Uganda pamoja na makampuni ya TotalEnergies na CNOOC hawakutoa ufafanuzi wowote kuhusu matamshi ya Bobi Wine.
Kuchelewa kwa uzalishaji wa mafuta
Akiba ya mafuta ya Uganda inakadiriwa kufikia mapipa bilioni 6.65. Mafuta hayo yaligunduliwa takribani miaka 20 iliyopita, lakini uzalishaji wake umechelewa mara kwa mara kutokana na mvutano kati ya makampuni ya kimataifa na serikali, pamoja na upinzani kutoka kwa wanaharakati wa mazingira.
Rais Yoweri Museveni, mwenye umri wa miaka 81, ameitawala Uganda kwa takribani miaka 40.
Bobi Wine amesema amepigwa mara mbili na vyombo vya usalama wakati wa kampeni na pia kuzuiwa kufanya kampeni katika baadhi ya maeneo ya nchi.
Kwa mujibu wa Boni Wine na Umoja wa Mataifa, mamia ya wafuasi wake wamekamatwa wakati wa kampeni. Serikali ya Uganda, kwa upande wake, imesema kuwa kukamatwa huko kunatokana na ukiukwaji halali wa sheria za jinai.
Comments
No comments Yet
Comment