Sport
Dollar
43,0411
0.01 %Euro
50,2797
-0.07 %Gram Gold
6.189,8900
0.49 %Quarter Gold
10.302,3900
-0.93 %Silver
105,9100
-2.26 %Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera, amemualika Rais wa Urusi Vladimir Putin kutembelea nchi yake, shirika la habari la serikali la Urusi TASS liliripoti siku ya Jumatano.
Rais mpya aliyechaguliwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera, amemualika Rais wa Urusi Vladimir Putin kutembelea nchi yake, shirika la habari la serikali la Urusi TASS liliripoti siku ya Jumatano.
Urusi imekuwa mshirika wa Touadera katika miaka ya hivi karibuni, huku 2018 CAR ikiwa nchi ya kwanza ya Afrika Magharibi na Kati kuwaleta mamluki wa Urusi Wagner kwa lengo la kukabiliana na makundi kadhaa ya waasi.
Touadera, aambaye amekuwa madarakani tangu 2016, alishinda muhula wa tatu, matokeo ya awali yalionesha wiki hii, na kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa urais uliofanyika Disemba 28.
Katika mahojiano kwa njia ya video na TASS, Touadera alisema Putin "alikuwa makini" kwa uhusiano na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Maslahi ya Urusi
Akizungumzia matokeo ya awali ya uchaguzi yaliyomuonesha Touadera anaongoza, kundi la Wagner liliandika kwenye mtandao wa Telegram: "Hatuna shaka njia iliyochaguliwa ya kuhakikisha utulivu na amani itakuwa sawa."
Ushindi wa Touadera unatarajiwa kuendeleza sera ya maslahi ya Urusi katika taifa hilo, ikiwemo uchimbaji wa madini ya dhahabu na almasi.
Comments
No comments Yet
Comment