Sport
Dollar
43,1388
0.21 %Euro
50,2459
-0.08 %Gram Gold
6.246,2500
0.83 %Quarter Gold
10.381,6000
0.77 %Silver
110,7700
4.07 %Jeshi la Sudan linasema operesheni ya angani na ardhini imeharibu mamia ya magari katika kipindi cha wiki moja iliopita
Jeshi la Sudan siku ya Ijumaa lilisema kuwa limewakabili vikali vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) wakati wa operesheni ya angani na ardhini katika kipindi cha wiki moja iliopita kwenye kanda za Darfur na Kordofan.
Katika taarifa, jeshi lilisema vikosi vyake vilifanya mashambulizi dhidi ya maeneo ya RSF, kuharibu magari 240 ya kivita na kuwaua mamia ya wapiganaji.
Jeshi limesema operesheni hiyo pia ililenga kile walichokiita maeneo ya RSF ya mikakati, ikiwemo sehemu wanazorushia ndege zisizo na rubani na ya kuhifadhi silaha, pamoja na maeneo katika Uwanja wa Ndege wa Nyala Kusini mwa Darfur.
Iliongeza kuwa wamefanikiwa kuwatimua wapiganaji wa RSF kutoka katika maeneo yote ya Darfur na Kordofan, na kwamba operesheni ilikuwa bado inaendelea kuwasaka wapiganaji waliobakia.
RSF hawajatoa taarifa yoyote kuhusu yaliyosemwa na jeshi.
Raia wameondolewa katika makazi yao
Mapigano yamezidi katika wiki za hivi karibuni kwenye majimbo matatu ya Sudan ya Kordofan – Kaskazini, Magharibi na Kusini – ambapo vita kati ya pande hizo mbili vimesababisha maelfu ya raia kukimbia makazi yao.
Hali mbaya kwa watu nchini Sudan imekithiri tangu vita kati ya jeshi la RSF kuzuka Aprili 2023 baada ya kutofautiana kuhusu muundo wa jeshi la pamoja, huku maelfu ya watu wakiuawa na mamilioni wakiondoka katika makazi yao.
Comments
No comments Yet
Comment