Dollar

38,8949

0.36 %

Euro

43,4533

-0.25 %

Gram Gold

3.997,1000

-0.9 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Familia hiyo iliyokuwa kizuizini tangu mapinduzo ya Agosti 2023, iliachiliwa kufuatia juhudi za kidiplomasia za serikali ya Angpla.

Rais Bongo wa Gabon aliyeondolewa madarakani akimbilia Angola na familia yake

Rais wa zamani wa Gabon aliyeondolewa madarakani Ali Bongo amesafiri kwa ndege hadi Angola pamoja na mkewe na mtoto wake wa kiume, ambao walikuwa wameachiliwa karibu miaka miwili baada ya kuzuiliwa kufuatia mapinduzi, ofisi ya rais wa Angola ilisema Ijumaa.

Familia ilikaribishwa "kwa sababu za kibinadamu," msemaji wa rais Luis Fernando alisema. "Halafu wataamua wanachotaka kufanya, kumaanisha, ni nchi gani wanataka kwenda kuishi kama watu walio uhamishoni," aliongeza.

Ofisi ya rais ilichapisha picha ambazo ilisema zilionyesha Bongo akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Luanda, maili 700 (1,100km) chini ya pwani ya magharibi mwa Afrika kutoka mji mkuu wa Gabon Alhamisi usiku.

Ilisema familia hiyo ilikuwa imeachiliwa baada ya uwakilishi wa kidiplomasia kutoka Angola.

Kizuizi cha nyumbani

Sylvia Bongo, 62, na mwanawe Noureddin, 33, waliwekwa chini ya ulinzi muda mfupi baada ya mapinduzi ya Agosti 2023 na kushtakiwa kwa uhalifu ikiwa ni pamoja na ubadhirifu na utakatishaji fedha.

Walihamishiwa kwenye kizuizi cha nyumbani mnamo Mei 9, vyanzo viwili vinavyofahamu kesi hiyo vilisema.

Hivi majuzi walikuwa wamezuiliwa katika vyumba vya chini ya ardhi katika ikulu ya rais huko Libreville, moja ya vyanzo vilisema.

Ali Bongo, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 66, awali aliwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani baada ya mapinduzi hayo, ingawa maafisa baadaye walisema alikuwa huru kuhama kama alivyotaka. Wafuasi wake walisema hilo si kweli.Wakili wa familia Francois Zimeray alithibitisha kuachiliwa kwao.

Wito wa AU

"Sylvia na Noureddin Bongo hatimaye wataweza kufungua ukurasa, kuponya na kujenga upya.

Tunapenda kuwashukuru wale wote ambao kwa njia moja au nyingine walishiriki katika matokeo haya," alisema. "Kutolewa huku ni matunda ya juhudi za muda mrefu za mahakama na kidiplomasia."

Maafisa wa Umoja wa Afrika walitoa wito wa kuachiliwa kwa mke wa Bongo na mwanawe mwezi uliopita.

Wafuasi wao wamesema waliteswa wakiwa kizuizini, ingawa kiongozi wa mapinduzi Brice Oligui Nguema, ambaye sasa anahudumu kama rais, amekanusha hilo.

Muhula mpya wa rais Nguema

Waziri wa mawasiliano wa Gabon, Paul-Marie Gondjout, hakujibu mara moja ombi la kutoa maoni yake.

Nguema aliapishwa kwa muhula wa miaka saba kama rais mwezi huu baada ya kushinda uchaguzi kwa karibu 95% ya kura.

Bongo alikuwa ametawala Gabon tangu 2009, akichukua nafasi ya babake, ambaye alifariki baada ya zaidi ya miongo minne madarakani.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#