Sport
Dollar
38,8949
0.36 %Euro
43,4533
-0.25 %Gram Gold
3.997,1000
-0.9 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Maureen Mabonga amehukumiwa miezi minane jela kwa kuhusika na 'mienendo ya uchochezi' ikiwemo 'kuchochea uasi' kwa misingi ya kikabila.
Maureen Mabonga, mbunge wa nchini Zambia wa chama tawala cha zamani Patriotic Front, amehukumiwa kifungo cha miezi minane gerezani siku ya Ijumaa kwa "mienendo ya uchochezi" ikiwemo "kuchochea uasi" kwa misingi ya kikabila.
Upande wa mashtaka ulikuwa umemuomba hakimu wa mahakama katika mji mkuu, Lusaka , kumpata na hatia Mabonga katika mashtaka mawili tofauti.
Hata hivyo, baada ya kusikiliza pande zote mbili, hakimu huyo alihukumu Mabonga afungwe jela kwa miezi minane na faini ya Kwacha za Zambia 1,600 (chini ya dola 100).
Mabonga, mbunge wa jimbo la Mfuwe mashariki mwa Zambia, ni mwanasiasa wa pili wa upinzani kukabiliwa na kifungo cha gerezani ndani ya mwezi mmoja, kufuatia kupatikana na hatia kwa Munir Zulu.
Kesi sawa na hiyo
Katika hukumu yake hakimu Kasanda alieleza kuwa Mabonga alitoa matamshi ya uchochezi ambayo yangeweza kusababisha uasi katika taifa kwa misingi ya kisiasa na kikabila.
Mabonga alishtumiwa kwa kutoa matamshi ya uchochezi mjini Lusaka mwezi Mei 2024, ambayo yalitafsiriwa kuwa uchochezi dhidi ya kabila fulani.
Mwezi Mei 2025, hakimu alimhukumu Munir Zulu, mbunge mwingine, kifungo cha miezi 18 jela katika kesi kama hiyo kufuatia matamshi aliyoyatoa katika mkutano na waandishi wa habari Septemba 2023.
Zulu alisisitiza kuwa Rais wa Zambia Hakainde Hichilema anatakiwa kulivunja bunge.
Uchaguzi mdogo
Kwa mujibu wa sheria za Zambia, mbunge yeyote anayepatikana na hatia anapoteza kiti chake cha ubunge, na uchaguzi mdogo katika eneo lake unafanyika ndani ya kipindi cha miezi mitatu.
Mabonga na wakili wake hawakuzungumza chochote baada ya hukumu hiyo, lakini wanaounga mkono chama chake walikusanyika nje ya mahakama kwa lengo la kumuonesha ushirikiano.
Comments
No comments Yet
Comment