Sport
Dollar
0,0000
%Euro
0,0000
%Gram Gold
0,0000
%Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Awali Sudan Kusini iliorodheshwa miongoni mwa mataifa ambayo yangefaidika kwa muda mnamo Oktoba 13, 2011, kulingana na mapigano nchini humo kati ya serikali ya rais Salva Kiir na makamu wake wa wakati huo Riek Machar.
Raia wa Sudan Kusini waliofurahia kinga maalum nchini Marekani sasa watahitajika kuondoka Marekani na kurejea nyumbani.
Raia 210 wa Sudan Kusini walikuwa Marekani chini ya mpango wa “Kinga ya muda”,yaani “Temporary Protected Status” ikiwa ni msamaha uliotolewa na Marekani kwa raia wa kigeni ambao hawawezi kurejea nyumbani kutokana na hali ya usalama katika mataifa yao ya asili.
Mara nyingi kinga hii hupewa raia wa nchi ambazo kuna mapigano, majanga ya kimazingira kama vile tetemeko la ardhi au kimbunga; au matatizo mengine ya muda.

Somalia, Sudan, Ethiopia, Cameroon na Sudan Kusini ni nchi barani Afrika ambazo zimengatiwa chini ya mpango huo.
Awali Sudan Kusini iliorodheshwa miongoni mwa mataifa ambayo yangefaidika kwa muda mnamo Oktoba 13, 2011, kulingana na mapigano nchini humo kati ya serikali ya rais Salva Kiir na makamu wake wa wakati huo Riek Machar.
Kwa hivyo Wasudan Kusini 210 walipewa hadhi ya kinga kwa muda na Marekani.
Sasa kipindi hicho kiliongezwa miaka ya 2013, 2014, na 2016, 2017 2019, na 2020.
Lakini kufikia Novemba 3, 2025 muda huo umefikia mwisho.
Serikali ya Marekani inasema baada ya kutathmini tena hali ya nchi na kushauriana na idara husika za Serikali ya Marekani, imebainika kuwa Sudan Kusini haikidhi tena vigezo vya kuwa katika mzozo unaoendelea ambao unatishia usalama wa raia wa Sudan Kusini wanaorejea kwao.
Ingawa kuna vurugu kati ya jamii zinazohusishwa na migogoro ya mipaka, mashambulizi ya kulipiza kisasi, na ubaguzi kwa misingi ya kikabila, inasema hakuna dalili kwa taifa hilo kuingia tena katika vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe.
Makubaliano ya mwaka 2018 ya kuunda serikali ya Mpito ya Umoja wa Kitaifa nchini Sudan Kusini yalikusudiwa kuandaa njia ya kurejea kwa amani na uchaguzi wa kwanza kabisa wa nchi hiyo tangu uhuru wake mwaka 2011, kuundwa kwa katiba mpya, mfumo wa mahakama pamoja na uwiano wa jeshi.
Lakini, miaka 7 baadaye yote haya hayajatokea.
Nchi hiyo changa barani Afrika inakabiliwa na mvutano mwingine baada ya Rais Salva Kiir kuamuru makamu wake wa rais Riek Machar akamatwe na kushtakiwa kwa mauaji, uhaini na uhalifu dhidi ya binadamu mnamo Septemba 2025.
Raia wa Sudan Kusini sasa watatarajiwa aidha kuondoka wenyewe, kupewa tiketi ya ndege, posho ya kuondoka ya $1,000 ili kuepuka kutimuliwa kwa nguvu.
Wataalamu nchini Sudan Kusini wanasema hatua hiyo ya Marekani ya kurejesha raia wa Sudan Kusini ni njia ya kulipiza kisasi kutokana na nchi hiyo kukataa kupokea kundi la pili ya wahamiaji wa Marekani nchini Sudan Kusini.
Comments
No comments Yet
Comment