Dollar

40,1751

0.23 %

Euro

47,0858

0.09 %

Gram Gold

4.345,9700

1.45 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Real Madrid, ambao ni mabingwa wa kihistoria wa Ulaya, walikubali kichapo cha magoli 4-0, mbele ya Paris Saint-Germain katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya klabu.

PSG ya Luis Enrique yaidhalilisha Real Madrid kwa kuichabanga mabao 4-0

Unaweza kusema kuwa Paris-Saint Germain walikuwa kwenye mazoezi yao ya kawaida tu.

 Ndio.

Machampioni wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Paris-Saint Germain ya Ufaransa, wameibamiza Real Madrid ya Hispania kwa mabao 4-0, katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu, uliyofanyika Julai 9, 2025 katika uwanja wa MetLife.

PSG, ambao bado wako kwenye fungate ya ushindi wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, waliendeleza pale pale walipoishia, baada ya kuwanyanyasa vilivyo, nyota wa Real Madrid waliokuwa wanaongozwa na mfaransa Kylian Mbappé akiwa na akina Vini Jr na Jude Bellingham.

Iliwachukua PSG ya kocha Luis Enrique kutoka Hispania, dakika sita tu ya mchezo kuanza kufungua ukurasa wa mabao, baada ya Fabian Ruiz kutumia makosa ya beki wa kati wa Real Madrid, Raúl Asencio na kumchambua vilivyo kipa Thibaut Courtois.

Tatizo la ubutu wa mabeki ni kama halijaisha hivi ndani ya Real Madrid, baada ya Antonio Rüdiger  kufanya fyongo katika dakika ya tisa ya mchezo, na kumpa mwanya Ousmane Dembélé kufanya kile alichozea kufanya mbele ya goli.

 PSG waliongeza bao lao la tatu katika dakika ya 24 kupitia kwa Fabian Ruiz, kabla ya Gonçalo Ramos, kushindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Real Madrid.

Mechi hiyo ilishuhudia nyota akina Mbappe na wenzake wakishindwa kufua dafu, huku mkongwe Luka Modric akiwaaga mashabiki wa Real Madrid kwa uchungu, akishiriki mchezo wake wa mwisho ndani ya Real Madrid, akiwa ameshinda mataji 28 katika michezo 597 ndani ya miaka 13, kwenye klabu hiyo.

Matokeo hayo yanaifanya PSG, kukutana na Chelsea ya Uingereza katika mchezo wa fainali utakaofanyika Julai 13, 2025.

 

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#