Sport
Dollar
38,7498
0.35 %Euro
43,6681
0.3 %Gram Gold
4.157,3500
1.3 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Kadinali Robert Prevost mzaliwa wa Marekani, amekuwa Papa wa kwanza katika historia ya Kanisa kutoka nchi hiyo.
“Ujumbe wa amani na upatanisho,” ndiyo ulikuwa msingi wa hotuba ya kwanza ya Papa wa 267 wa Kanisa Katoliki ambae matokeo ya uchaguzi wake yamepokelewa kwa shangwe na vifigo.
Kadinali Robert Prevost mwenye miaka 69, ni mzaliwa wa Marekani ambae anaweka historia ya kwanza ya kuwa Papa wa Kanisa Katoliki kutoka nchi hiyo. Jina lake la kipapa ni Leo XIV, akilichukua kutoka kwa Papa Leo III aliyetambulika kama "Papa wa Jamii na wa Wafanyakazi."
Safari yake ilianza 1982 alipotawazwa kama padre ambapo alihudumu kwa takriban miongo miwili nchini Peru ambapo pia alipata uraia wa nchi hiyo. Kati ya 1999 na 2014, Prevost alihudumu Chicago Marekani.
Mwaka wa 2014 Papa Francis alimteuwa kuwa askofu wa Chiclayo huko Peru. Alitawazwa kama askofu mkuu Januari 2023 na baada ya miezi michache Papa Francis akamuinua kuwa kadinali.

Hapo Papa Francis alimpa jukumu la kuongoza ofisi inayochunguza uteuzi wa maaskofu kutoka duniani kote, mojawapo ya kazi muhimu zaidi katika Kanisa Katoliki.
Kwa hivyo, ni dhahiri kwamba Kadinali Prevost hakuwa mgeni kwa makadinali wenzake 132 ambao alikuwa nao katika mchakato wa kumpigia kura papa mpya.
Papa Francis alionyesha imani kwake kwa kumpa vyeo tofauti kanisani, naye aliunga mkono mabadiliko ambayo Papa Francis aliyafanya kanisani pamoja na maadili yake ya usawa, haki kwa wahamiaji na kulegeza masharti ya kanisa kwa ajili ya kushirikisha zaidi mabara tofauti.

Na yeye si mgeni Afrika.
Katika wadhifa wake wa awali alitembelea nchi kama Kenya, Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Papa Leo XIV anapochukua uongozi wa zaidi ya waumini bilioni 1.4 wa Kanisa hilo, wengi wanasubiri kuona iwapo sera zake zitafanana na mtangulizi wake za kujaribu kuleta usawa na kupaza sauti za wanyonge.
Comments
No comments Yet
Comment