Sport
Dollar
42,8515
0.01 %Euro
50,9195
0.01 %Gram Gold
6.170,8800
0 %Quarter Gold
10.216,8600
-0.28 %Silver
99,0800
0.11 %Papa Leo XIV alitoa mfano wa moja kwa moja kuhusu simulizi za Krimasi na familia za watu wa Palestina zinazoishi kwenye mahema huku kukiwa na vita na wengine kuondoka katika makazi yao Gaza
Papa Leo alieleza kusikitishwa na madhila ya Wapalestina huko Gaza katika mahubiri yake ya Krismasi siku ya Alhamisi, alitoa wito katika ibada ya Krismasi wakati kote duniani wakisherehekea siku ya kuzaliwa Yesu.
Leo, papa wa kwanza Mmarekani, amesema simulizi ya Yesu kuzaliwa katika zizi kunaonesha Mungu "alikita hema lake" miongoni mwa watu wa dunia.
"Inakuaje, sasa, hatuwezi kuangazia mahema ya Gaza, ambayo yanapitia matatizo ya mvua kwa wiki kadhaa, upepo na baridi?" aliuliza.
Leo, akisherehekea Krismasi yake ya kwanza tangu kuchaguliwa mwezi Mei na makadinali wa dunia kumrithi Papa Francis, mtindo wake ni wa kutulia, na kutumia diplomasia zaidi kuliko mtangulizi wake na mara nyingi hujiepusha kutoa kauli za kisiasa katika mahubiri yake.
Lakini papa huyu mpya pia ameeleza kusikitishwa na hali ya Wapalestina huko Gaza mara kadhaa katika siku za hivi karibuni na kuwaambia waandishi wa habari mwezi uliopita kuwa suluhu pekee ya mzozo huo wa miongo kadhaa kati ya Israel na watu wa Palestina lazima kuwepo na taifa la Palestina.
Israel na Hamas walikubaliana kusitisha mapigano mwezi Oktoba baada ya miaka miwili ya mauaji ya halaiki ya Israel huko Gaza, lakini mashirika ya misaada yanasema bado misaada inayoingia Gaza ni kidogo sana, sehemu ambayo watu wake wote hawana makazi.
Katika ibada ya Alhamisi ambapo maelfu ya waumini walikuwepo katika Kanisa la St. Peter's Basilica, Leo pia alizungumzia hali ya watu wasiokuwa na makazi kote duniani na uharibifu unaosababishwa na vita maeneo mbalimbali duniani.
"Hali tete ndiyo iko kwa watu wanaoshindwa kujitetea, wamepitia vita vingi, vinavyoendelea na vya zamani, kusababisha kuwepo kwa vifusi na makovu," alisema papa.
"Hali hii inafanya vijana kulazimika kuchukuwa silaha, na kupigana bila kuelewa wanachohitajika kufanya huku kukiwa na hotuba za kujisifu za wale ambao wamewatuma katika uwanja wa vita kukutana na umauti," alisema.
Baadaye siku ya Alhamisi atatoa ujumbe unaowasilishwa kwa mwaka mara mbili "Urbi et Orbi" (kwa mji huo na dunia nzima) na baraka, ambao kwa kawaida ujumbe huo unaangazia migogoro duniani.
Comments
No comments Yet
Comment