Sport
Dollar
40,6911
0.04 %Euro
47,1373
0.04 %Gram Gold
4.411,7200
-0.21 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Silaha za nyuklia ni usaliti kwa uumbaji,' alisema Baba Mtakatifu huyo.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo wa 14, siku ya Jumanne aliadhimisha kumbukumbu ya miaka 80 toka liangushwe bomu la atomiki kwenye mji wa Hiroshima nchini Japan, akitoa rai kwa jumuiya ya kimataifa kurudia ahadi ya kulinda amani ulimwenguni.
Kulingana na Papa Leo wa 14, matumizi ya silaha za kinyuklia ni dhihaka kwa uumbaji wa Mungu.
"Silaha za kinyuklia ni dhihaka kwa ubinadamu na usaliti wa uumbaji ambao tunapaswa kuulinda," alisema Baba Mtakatifu katika taarifa yake.
Ujumbe wake unakuja wakati Japan na ulimwengu mzima, unaadhimisha miaka 80, tangu kutokea kwa mashambulizi kwenye miji ya Hiroshima na Nagasaki, na kusababisha vifo vya watu kati ya 150,000 na 246,000, mwisho wa mwaka 1945.
Comments
No comments Yet
Comment