Sport
Dollar
42,9304
0.18 %Euro
50,5746
-0.17 %Gram Gold
6.233,6600
1.02 %Quarter Gold
10.251,8200
0.34 %Silver
103,3400
4.29 %Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani alitumia fursa hiyo kukemea ubatili.
Papa Leo wa 14 ameadhimisha Ibada yake ya kwanza ya mkesha wa Krismasi, kama Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani.
Ibada hiyo ilifanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro huko Vatican jijini Roma, likihudhuriwa na makardinali, maaskofu, wawakishilishi wa kidiplomasia, mapadre na wageni mbalimbali.
Katika homilia yake, Papa Leo wa 14 alikemea ubatilli, akisema kuwa haipendezo kuona watu wakichukuliwa kama bidhaa.
Kabla ya kuanza kwa ibada hiyo, Baba Mtakatifu huyo aliwasalimia waamini waliokuwa wamejaa kwenye viunga vya Mtakatifu Petro, akiwatakia Heri ya Sikukuu ya Noeli.
Tofauti na mtangulizi wake, Papa Leo alianza kuadhimisha ibada ya mkesho muda mchache kuelekea saa sita usiku, huku akiendesha ibada hiyo kwa muda mrefu.
Baadhi ya vyombo vya habari vimechukulia hatua hiyo kama marejeo ya desturi za zamani za kanisa hilo.
Siku ya Alhamisi, ambayo ndiyo Krismasi yenyewe, Baba Mtakatifu atawasilisha ujumbe maarufu wa "Urbi et Orbi", ambao utaangazia mambo mbalimbali ulimwenguni.
Papa Leo wa 14, ambaye jina lake halisi ni Robert Francis Prevost alichaguliwa Mei 8, 2025 kama kiongozi wa 267 wa Kanisa Katoliki duniani, kufuatia kifo cha Papa Francis kilichotokea Aprili 21, 2025.
Comments
No comments Yet
Comment