Dollar

42,2134

0.24 %

Euro

48,8967

0.3 %

Gram Gold

5.430,7100

0.77 %

Quarter Gold

9.213,2100

0.59 %

Silver

65,6700

0.98 %

Robert James Purkiss aliyekamatwa huko Tidworth, Wiltshire mnamo 6 Novemba na alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu ya Westminster siku ya Ijumaa na huenda akarejeshwa Kenya kujibu mashtaka

Mwanajeshi wa Uingereza akamatwa kwa mauaji ya mwanamke wa Kenya mwaka 2012

Mwanajeshi wa zamani wa Uingereza anakabiliwa na kurejeshwa nchini Kenya kuhusiana na madai ya mauaji ya mwanamke mwenye umri wa miaka 21 mwaka wa 2012.

Shirika la Kitaifa la Uhalifu (NCA) lilisema Robert James Purkiss alikamatwa huko Tidworth, Wiltshire mnamo 6 Novemba na alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu ya Westminster siku ya Ijumaa.

Alikamatwa na maafisa wa Kitengo maalum cha kitaifa cha kuwahamisha washukiwa NCA kuhusiana na mauaji ya Agnes Wanjiru baada ya kibali kutolewa mnamo Septemba, shirika hilo liliongeza.

Purkiss, mwenye umri wa miaka 38, aliambia mahakama kwamba alinuia kupinga kurejeshwa kwake na aliwekwa rumande kabla ya kufikishwa kwake tena katika mahakama hiyo tarehe 14 Novemba.

Mawakili wake waliambia mahakama kwamba "anakanusha vikali" mauaji. Mwili wa Bi Wanjiru uligunduliwa kwenye tanki la maji taka karibu na hoteli moja katika mji wa Nanyuki, takriban maili 124 (200km) kaskazini mwa Nairobi, miezi mitatu baada ya kutoweka mnamo Machi 31, 2012.

Alikuwa na mtoto wa miezi mitano wakati huo.

Usiku aliouawa, inasemekana alikuwa kwenye baa na marafiki zake ambapo wanajeshi wa Uingereza pia walikuwepo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#