Dollar

40,1756

0.23 %

Euro

47,0548

0.04 %

Gram Gold

4.331,4800

1.11 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Mazungumzo kati ya DRC na kundi la waasi la M23 nchini Qatar "yanaendelea vizuri", mwanadiplomasia ameiambia AFP.

Mazungumzo ya DRC-M23 'yanaendelea vizuri': Mwanadiplomasia

Mazungumzo kati ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo na kundi la waasi la M23 "yanaendelea vizuri", mwanadiplomasia ameiambia AFP siku ya Alhamisi baada ya wajumbe kukutana nchini Qatar.

Wiki iliopita waasi wa M23 walitaka kuwepo kwa mazungumzo zaidi kujadili masuala ambayo hayakujumuishwa kwenye makubaliano ya amani yaliyotiwa saini kati ya Rwanda na DRC jijini Washington mwezi Juni kumaliza mapigano ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu mashariki mwa DRC.

Wajumbe kutoka serikali ya DRC na M23 walikuwa wanafanya kazi pamoja na wapatanishi wa Qatar "kutatua masuala yaliyobakia", mwanadiplomasia huyo alisema kwa masharti kuwa asitambulishwe kutokana na namna mazungumzo hayo yalivyo nyeti.

Wajumbe wanataka "kumaliza mateso wanayopitia watu, kuhakikisha kusitishwa kwa mapigano, na kupendekeza hatua zaidi kuchukuliwa katika kuleta upatanishi", mwanadiplomasia huyo aliongeza.

Makubaliano tofauti ya kusitisha mapigano

Makubaliano hayo yaliyotiwa saini kati ya DRC na Rwanda yalikuwa yanalenga kumaliza mapigano ambayo yamesababisha mauaji ya maelfu ya watu katika eneo la mashariki mwa DRC lenye utajiri wa madini.

Lakini M23, kundi kubwa linalokabiliana na wanajeshi wa DRC, hawakuwepo kwenye mazungumzo ya Washington na kutaka kuwepo kwa majadiliano tofauti ya kusitisha mapigano na serikali ya DRC.

M23 ilidhibiti maeneo makubwa mwezi Januari na Februari, ikiwemo miji muhimu ya Goma na Bukavu.

Kumekuwa na mapigano makali mashariki mwa DRC kwa zaidi ya miongo mitatu, na kusababisha maelfu ya watu kuondoka katika makazi yao.

Nchi ya Rwanda inakanusha kuunga mkono kundi la waasi la M23, lakini wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasema kuwa Rwanda "imekuwa na jukumu kubwa" katika mashambulizi ya M23, ikiwemo katika makabiliano.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#