Dollar

40,5963

0.02 %

Euro

46,5245

0.4 %

Gram Gold

4.297,7200

0.56 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Miongoni mwa makampuni yanayomilikiwa na serikali KPC imedumisha faida kubwa lakini inasalia kutatizwa na uzembe katika urasimu.

Mawaziri waidhinisha ubinafsishwaji wa kampuni ya usambazaji mafuta Kenya - KPC

Baraza la Mawaziri nchini Kenya limeidhinisha ubinafsishaji wa sehemu ya Kampuni ya Kenya Pipeline (KPC), na hivyo kufungua njia kwa Wakenya kununua hisa katika kampuni hiyo.

Kampuni hiyo sasa itaorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Nairobi (NSE) ambapo katik ahatua wanayonuia itafungua uwezo kamili wa kibiashara wa kampuni hiyo.

‘‘Hii ni sehemu ya mabadiliko mapana ya sera yanayolenga kupunguza jukumu la serikali katika biashara na kuwezesha sekta ya kibinafsi kuchukua uongozi katika kusukuma ukuaji, ufanisi na uvumbuzi,’’ ilisema sehemu ya mawasiliano kutoka kwa baraza hilo.

Miongoni mwa makampuni yanayomilikiwa na serikali KPC imedumisha faida kubwa lakini inasalia kutatizwa na uzembe katika urasimu.

Kuiga mifano ya makampuni mengine

Uamuzi huo ulifikiwa wakati wa kikao cha Baraza la Mawaziri kilichoongozwa na Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi.

Baraza la Mawaziri lilisisitiza kuwa mkakati huu unatokana na mifano ya mafanikio katika vyombo vingine.

"Baraza la Mawaziri lilikumbushwa kwamba hatua kama hizo hapo awali zimeleta matokeo ya mageuzi. Safaricom, Kenya Commercial Bank, na KenGen ni mifano mikuu ya mashirika ya zamani yaliyokuwa yakidhibitiwa na serikali ambayo yalikuja kuwa makampuni yaliyofanya vizuri kufuatia ubinafsishaji, kuinua thamani ya wanahisa, kupanuka kikanda, na kutengeneza maelfu ya nafasi za ajira."

Ubinafsishaji wa KPC, unatarajiwa kuongeza imani ya wawekezaji na kusaidia maendeleo ya masoko ya mitaji ya Kenya.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#