Sport
Dollar
40,6571
0.04 %Euro
47,0001
1.04 %Gram Gold
4.371,8900
1.68 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Hatua hiyo inalenga kupambana na uhalifu wa kifedha na kurejesha imani ya umma katika taasisi za fedha, Benki Kuu ya Somalia imesema.
Benki Kuu ya Somalia imetangaza sera mpya inayowataka raia kuwasilisha vitambulisho vyao vya kitaifa kabla ya kupata huduma za kibenki.
Hatua hiyo inalenga kupambana na uhalifu wa kifedha na kurejesha imani ya umma kwa taasisi za fedha, Benki Kuu imesema.
Hatua hii, itaathiri huduma za benki kama vile kufungua akaunti, kufanya malipo, kuweka na kutoa pesa na kuomba mikopo.
"Kanuni hiyo inalenga kukomesha ulaghai wa matumizi ya vitambulisho, kuzuia utoroshaji wa pesa, na kuhakikisha upatikanaji salama wa huduma za kifedha," Benki Kuu ya Somalia imesema.
Somalia haikuwa na mfumo wa vitambulisho kwa zaidi ya miaka 30 kufuatia kuanguka kwa serikali ya aliyekuwa rais Siad Barre mnamo Januari 1991.
Katika kipindi hicho cha muda, miamala ya kifedha, huduma za serikali na hata utekelezaji wa sheria ulitegemea kuaminiana, mitandao ya koo au pasi za kusafiria za kigeni bila kuwa na utambulisho rasmi.
Nchi ilizindua utoaji wa kadi mpya za utambulisho wa kibayometriki mwezi Septemba 2023.
Hii imesambaa katika mji mkuu, Mogadishu, hadi Galmudug, Hirshabelle, na hata Las Anod katika eneo la SSC-Khaatumo.
Kanuni mpya ya huduma za benki ilitolewa kwa ushirikiano na Mamlaka ya Kitaifa ya Vitambulisho na Usajili (NIRA) na Chama cha Mabenki cha Somalia.
Hapo awali itaanza kutekelezwa katika eneo la Benadir, ambalo linajumuisha mji mkuu Mogadishu, kabla ya kusambazwa kote nchini.
Ni sehemu ya mpango wa mabadiliko ya kitaifa wa Somalia, uliopitishwa Machi 2025, ambao unalenga kujenga upya mifumo ya serikali, kuweka huduma za serikali kidigitali na kuimarisha utu wa raia.
Serikali imetunga sheria za ulinzi wa taarifa na kutoa wito kwa watoa huduma wote wa serikali na wasio wa kiserikali kuunganisha huduma - ikiwa ni pamoja na elimu, afya, na ruzuku - na mfumo wa vitambulisho vya kitaifa.
"Mfumo huu wa vitambulisho unashughulikia matatizo mengi ya muda mrefu, kutoka kwa uchaguzi na uhamaji hadi usalama wa umma na fursa za kiuchumi," Waziri Mkuu Hamza Abdi alisema wakati huo.
Comments
No comments Yet
Comment