Maandamano hayo, ambayo ni ya vurugu kuwahi kutokea kwa takriban miongo mitatu, yamesababisha watu wasiopungua 188 kukamatwa.

Mauritius yaondoa marufuku ya kutotoka nje usiku baada ya ufyatuaji wa polisi kusababisha maandamano

Mauritius imeondoa marufuku ya kutotoka nje usiku iliyotangazwa wiki iliopita baada ya maandamano kutokea katika taifa hilo la kisiwa.

Ofisi ya Waziri Mkuu Navin Ramgoolam, siku ya Jumatatu, ilisema hatua hiyo inafuata kuimarika kwa hali.

“Marufuku ya mwisho ilimalizika saa Kumi Unusu alfajiri Jumatatu Oktoba 19, na muda haujaongezwa,” Ofisi ya Ramgoolam ilisema.

Maandamano hayo, mabaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha karibu miongo mitatu, yalisababisja watu wasiopungua 188 kukamatwa na kushtakiwa kwa uporaji, kuchoma moto, uharibifu wa vituo vya polisi na kuwa na vilipuzi .

Maandamano yalianza kutokana na uhaba wa maji na kuongezeka kwa gharama za maisha, lakini vurugu ziliendelea baada ya afisa wa polisi kumpiga risasi na kumjeruhi mwanamke mmoja.

Ofisa huyo baadaye alikamatwa na kufikishwa mahakamani.

“Barabara zimefunguliwa, shule zote zimefunguliwa tena huku masomo yakiendelea kama kawaida, na maisha kurudi kama ilivyokuwa," Wasimamizi wa masuala ya Utalii wa Mauritius walisema katika taarifa nyingine.

#