Hadi kufariki kwake mwaka 1986, Machel alikuwa anapinga vikali utawala wa kikoloni.

Afrika Kusini, Msumbiji kumuenzi rais wa zamani Machel miaka 40 baada ya ajali ya ndege

Aliyekuwa rais wa Msumbiji na mpigania uhuru Samora Machel atakumbukwa siku ya Jumatatu katika hafla ya pamoja siku ya Jumatatu na Afrika Kusini na Msumbiji kuadhimisha miaka 40 tangu alipofariki katika ajali ya ndege.

Maadhimisho hayo yatafanyika katika eneo la Mbuzini, sehemu ya Afrika Kusini katika mkoa wa Mpumalanga karibu na eneo lilipotokea ajali hiyo.

Machel alikuwa kiongozi wa Msumbiji baada ya nchi hiyo kupata uhuru kutoka kwa utawala wa Ureno mwaka 1975 hadi kufariki dunia 1986.

Uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo ya ndege iliyomuua Machel na watu wengine 34 ulibaini kuwa marubani walikuwa na makosa, lakini miaka 40 baada ya kifo chake, bado kuna maswali kuhusu nini hasa kilichotokea.

Nini Kilitokea Oktoba 18, 1986?

Siku hii, Machel alifariki pamoja na baadhi ya mawaziri wake, waandishi wa habari na wahudumu wakati ndege waliokuwemo ndani kupata ajali kaika Milima ya Lebombo eneo la Afrika Kusini la Mbuzini karibu na mpaka wa Msumbiji na Eswatini.

Walikuwa wanarudi kutoka kwenye mkutano wa viongozi wa kanda nchini Zambia.

Uchunguzi ulioongozwa na Afrika Kusini kuhusu ajali hiyo uliwalaumu marubani kwa ajali hiyo na kubaini kuwa hakukuwa na njama yoyote.

Afrika Kusini inasema kuwa hafla ya Jumatatu ya kumuenzi Machel itafanyika chini ya mada : “Kukumbuka Kujitolea kwa muda mrefu kwa Watu wa Kusini mwa Afrika: Kuwaenzi Wote Waliofariki katika Mkasa wa Mbuzini”.

#