Waasi wa Tigray walianzisha mashambulizi dhidi ya serikali kuu mwezi uliopita, lakini walikabiliwa vikali na wakapoteza udhibiti wa jimbo hilo.
Huku waasi wakiondoka katika maeneo ya jimbo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray, meya wa mji mkuu wa eneo hilo aliyetuliwa na serikali kuu ameiambia AFP siku ya Jumatatu kuwa watafanya uchaguzi katika kipindi cha miezi sita ijayo.
Waasi wa Tigray, ambao wamekuwa wakidhbiti kanda hiyo kwa muda mrefu, walianzisha mashambulizi dhidi ya serikali kuu mwezi uliopita, lakini walikabiliwa na kupoteza udhibiti wa jimbo hilo.
Vita hivyo vilizua hofu ya kuwepo kwa mapigano ya kikanda, lakini waasi walilazimika kuondoka hapo baada ya kushambuliwa kwa droni.
Siku ya Ijumaa, serikali ya Ethiopia ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed iliteuwa uongozi mpya wa mpito Tigray, eneo lenye watu karibu milioni sita, ukiwa na majukumu ya kufanya uchaguzi na kuwapa makazi wale walioondolewa katika makazi yao.
Kuhakikisha usalama
"Jukumu letu ni kuandaa mazingira mazuri kwa ajili ya uchaguzi kwa kuhakikisha kuna amani na usalama kote Tigray," Shishay Amare, meya mpya wa mji mkuu wa jimbo Mekelle, aliiambia AFP.
"Nina imani kuwa hili litafanyika ndani ya miezi sita, kulingana na mpango," aliongeza.
Tigray haikushiriki katika uchaguzi wa wabunge wa nchi nzima uliofanyika mwezi Juni, ambapo chama cha Abiy cha Prosperity kilirudi madarakani kwa ushindi mkubwa.
Karibu watu milioni moja wameondolewa kwenye makazi yao kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe kaskazini mwa Ethiopia kati ya 2020-2022, ambavyo vilisababisha vifo vya watu karibu 600,000, kulingana na makadirio ya Umoja wa Afrika.
Meya mpya wa mji wa Mekelle anasema suala nyeti la eneo la Magharibi mwa Tigray -- ambalo linagombaniwa na Tigray na jimbo jirani la Amhara -- litaanganziwa katika siku za baadaye.

