Tahadhari hiyo, imeangazia sababu mbalimbali, zikiwemo za kiafya, kiuhalifu, utekaji nyara, ugaidi, machafuko na usalama barabarani.

Marekani yaongeza tahadhari ya kusafiri Kenya

Serikali ya Marekani imepandisha kiwango cha tahadhari kwa raia wake wanaopanga kusafiri kwenda Kenya.

Kulingana na serikali ya nchi hiyo, tahadhari hiyo, imeongezeka kutoka kiwango cha kwanza hadi cha pili, ikiashiria kuwa wasafiri wanashauriwa kutathmini upya mipango yao ya safari kutokana na hatari zilizotajwa na serikali hiyo.

Tahadhari hiyo, imeangazia sababu mbalimbali, zikiwemo za kiafya, kiuhalifu, utekaji nyara, ugaidi, machafuko na usalama barabarani.

Siku chache zilizopita, Kenya ilitangaza ongezeko la maambukizi ya Ebola, ambapo hadi kufikia sasa, jumla ya watu 8, wamethibitika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo.

Mlipuko huo, ulianza, baada ya raia mmoja wa Kenya aliyekuwa akiishi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kusafiri kwa barabara kupitia Uganda na kisha kusafiri kwa ndege hadi Nairobi, ambapo alifariki dunia Oktoba 5, 2026.

Vipimo vya maabara, vilithibitisha kuwa alikuwa ameambukizwa virusi vya Ebola vya aina ya Bundibugyo.

#