Sport
Dollar
41,3293
0.18 %Euro
49,1107
0.15 %Gram Gold
4.902,6900
0.21 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Kulingana na Alexander Muteti, ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Nairobi, kulikuwa na sababu za kutoa hati ya kukamatwa kwa mshukiwa huyo ambaye ni mkazi wa Uingereza.
Mahakama ya jijini Nairobi, siku ya Jumanne iliwasilisha hati ya kukamatwa kwa raia wa Uingereza anayehusishwa na mauaji ya binti wa Kikenya, ambaye mwili wake uliopolewa kutoka shimo la maji machafu, zaidi ya miaka kumi iliyopita.
Agnes Wanjiru, alifariki dunia mwaka 2012, baada ya kuripotiwa kutoka kwenye starehe akiwa pamoja na askari wa Uingereza katika mji wa Nanyuki ambako wanajeshi hao wameweka ngome yao.
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) ilisema kuwa ushahidi uliokusanywa, unamhusisha askari huyo katika mauaji hayo.
Kulingana na Alexander Muteti, ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Nairobi, kulikuwa na sababu za kutoa hati ya kukamatwa kwa mshukiwa huyo ambaye ni mkazi wa Uingereza.
Comments
No comments Yet
Comment