Dollar

40,6150

-0.1 %

Euro

47,3707

-0.23 %

Gram Gold

4.424,9900

0.5 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Eneo hilo, ambalo linahifadhi zaidi ya wakimbizi 395,000 - wengi wao kutoka Sudan Kusini katika kambi saba - linashuhudia ongezeko la utapiamlo kwa watoto, ugonjwa wa malaria, na wagonjwa kulazwa.

Kambi za wakimbizi Gambella, Ethiopia zakosa rasilimali za kutosha

Kambi za wakimbizi katika eneo la Gambella nchini Ethiopia zinakabiliwa na janga kubwa la kibinadamu kufuatia kupunguzwa kwa misaada ya kimataifa ambayo imelemaza huduma muhimu, ikiwa ni pamoja na usambazaji wa chakula, huduma za afya, na kukabiliana na magonjwa.

Kambi hiyo iko kusini-magharibi mwa Ethiopia karibu na mpaka wa Sudan Kusini.

“Gambella imehifadhi idadi kubwa ya wakimbizi wengi wa Sudan Kusini tangu 2014. Leo, zaidi ya wakimbizi 395,000 wanaishi katika kambi saba,” Shirika la Médecins Sans Frontières (MSF) limesema.

Kupungua kwa kasi kwa usaidizi wa kibinadamu, kutokana na kupunguzwa kwa ufadhili wa kimataifa kutoka kwa wafadhili wakuu kama vile USAID, tayari kumelazimisha kusimamishwa kwa mipango ya lishe.

“Lishe imesimamishwa katika kambi nne kati ya saba za wakimbizi, na kuacha karibu watoto 80,000 walio chini ya umri wa miaka mitano katika hatari ya utapiamlo unaotishia maisha.”

Wakimbizi wanalalamika kuwa hawana mahitaji ya kutosha.

"Tunapokea chakula mara moja kwa mwezi-mahindi, ngano, na mtama-lakini kila mara huisha kabla ya mwezi kuisha," alisema Nyauahial Puoch, mama wa watoto watano ambaye binti yake mwenye umri wa miezi 17 alilazwa katika kituo cha lishe cha wagonjwa cha MSF huko Kule. "Baadhi ya vitu tulivyokuwa tukipata havitolewi tena."

Tangu Oktoba 2024, wakimbizi katika kambi ya Kule wameripotiwa kupokea kalori 600 kwa siku—chini ya asilimia 30 ya kiwango cha chini kinachopendekezwa.

Usambazaji wa chakula katika kambi nyengine pia umetatizwa, huku nyengine zikienda kwa miezi bila kufanya kazi kwa sababu ya masuala ya ugavi na upungufu wa fedha. Athari kwenye lishe ya watoto ni kubwa.

MSF iliripoti ongezeko la asilimia 55 ya watoto wanaolazwa katika mpango wake wa lishe ya matibabu mwaka huu ikilinganishwa na 2024.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#