Dollar

40,6834

0.04 %

Euro

47,6866

0.3 %

Gram Gold

4.417,1900

0.32 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Ama kwa upande wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, ambae ndie Makamu wa Rais wa Kwanza wa sasa Zanzibar, amependekezwa kugombea nafasi ya Urais.

ACT Wazalendo yapendekeza majina ya wagombea urais Tanzania bara na Zanzibar

Chama cha upinzani nchini Tanzania ACT Wazalendo, kupitia Halmashauri Kuu yake, kimependekeza majina ya wagombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar.

Kwa Tanzania Bara, waliopendekezwa ni Aaron Kalikawe na Luhanga Mpina.

Ama kwa upande wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, ambae ndie Makamu wa Rais wa Kwanza wa sasa Zanzibar, amependekezwa kugombea nafasi ya Urais.

Majina hayo, yatawasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Taifa kwa ajili ya kupigiwa kura.

Ikumbukwe kuwa, haya ni maandalizi ya vyama mbali mbali vya kisiasa nchini humo ya kuchagua viongozi wao katika nafasi ya urais, ubunge na udiwani watakao peperusha bendera za vyama vyao kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.

Tayari Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania imetenga Agosti 9-27 kama tarehe za utoaji fomu kwa wagombea wa kiti cha urais na makamu, huku Agosti 14-27 zikiwa ni siku za utoaji fomu kwa wagombea wa ubunge na udiwani.

Kwa mujibu wa Tume hiyo, Agosti 27 ni siku ya kurudisha fomu kwa wagombea wote.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#