Dollar

40,7086

0.17 %

Euro

47,4348

-0.19 %

Gram Gold

4.444,4400

0.22 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Hatua hiyo inafuatia Azimio la Ankara lililotiwa saini Disemba 2024 ambalo lilipunguza mvutano kuhusu mkataba wa Ethiopia na Somaliland wa ufikiaji wa bahari.

Ethiopia yamteua mjumbe mpya nchini Somalia baada ya mvutano wa kidiplomasia

Balozi mpya wa Ethiopia nchini Somalia, Suleiman Dedefo, amewasilisha rasmi hati zake za utambulisho kwa Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, kuashiria hatua ya kurudisha uhusiano wa kawaida baada ya miezi kadhaa ya mvutano wa kidiplomasia.

Mzozo huo uliochochewa na Ethiopia kutia saini mkataba wa maelewano na Somaliland, eneo lililojitenga la Somalia, mnamo Januari 2024.

Makubaliano hayo yalikuwa na lengo la kuipa Ethiopia ufikiaji wa Bahari Sham kupitia ufuo wa Somaliland na baadaye Ethiopia kuitambua Somaliland kama nchi huru, pamoja na makubaliano yanayohusiana na usalama.

Somalia, ambayo inaitambua Somaliland kama sehemu ya ardhi yake huru, ilikataa mpango huo na kusema ni ukiukaji wa uhuru wa eneo lake.

Uhusiano wa kidiplomasia uliendelea kuzorota hadi mwezi Disemba 2024, wakati Ethiopia na Somalia zilipotia saini Azimio la Ankara, makubaliano yaliyosimamiwa na Uturuki ambayo yalisaidia kupunguza mvutano na kuweka msingi wa mazungumzo mapya.

Azimio hilo lilijumuisha ahadi za kuheshimu uhuru wa kila mmoja na kuendeleza mazungumzo ya kiufundi juu ya suluhu ya Ethiopia kufikia bahari.

"Nilipata heshima ya kuwasilisha barua yangu ya utambulisho kwa Mheshimiwa Rais Hassan Sheikh Mohamud, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Somalia," Balozi Dedefo alisema.

"Katika hafla hiyo, tulijadili kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kukuza uhusiano wa kiuchumi na kuimarisha ushirikiano wa usalama.

Uteuzi wa balozi mpya unatazamwa kama sehemu ya juhudi pana za kujenga upya uaminifu kati ya majirani wa Pembe ya Afrika, ambao wameanza tena mazungumzo ya hali ya juu na kuahidi kushughulikia masuala yaliyosalia.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#