Sport
Dollar
42,3350
0.2 %Euro
49,1712
0.05 %Gram Gold
5.547,4900
-0.07 %Quarter Gold
9.430,0100
0 %Silver
69,2000
0.51 %Jehsi la Sudan mjini Babnousa vimekabili na kurudisha nyuma shambulio la wapiganaji wa RSF huku mapigano makali yakiendelea katika majimbo yote ya Kordofan.
Jeshi la Sudan limefanikiwa kuyazima mashambulizi mapya ya wapiganaji wa RSF dhidi ya mji wa Babnousa uliopo Kordofan Magharibi, kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi.
Chanzo hicho, ambacho hakikutaka kutajwa kwa jina, kiliiambia shirika la habari la Anadolu sikiu ya Jumatatu kwamba wanajeshi wa kikosi maalim waliwarudisha nyuma wapiganaji wa RSF waliovamia mji huo kwa kutumia silaha nzito na hafifu.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, jeshi liliisababishia RSF “hasara kubwa ya watu na vifaa.”
Hakujatolewa taarifa rasmi kutoka jeshi la Sudan wala RSF kuhusu tukio hilo.
RSF ilisema Jumapili kwamba wapiganaji wake walikuwa wakisonga kuelekea Babnousa ili kuudhibiti mji huo, ambao umekuwa umezingirwa tangu Januari 2024.
Katika siku za karibuni, jeshi limezuia mashambulizi kadhaa ya RSF kwa kutumia mashambulizi ya mizinga, ndege zisizo na rubani na magari ya kivita, kwa mujibu wa taarifa za ndani.
Jeshi pia limekuwa likisambaza mahitaji muhimu kwa wanajeshi wake walioko ndani ya mji huo, ambao sasa hauna raia baada ya wakazi 177,000 kukimbia, kamati za misaada za eneo hilo zilisema.
Mwezi uliopita, RSF iliteka Al Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, na ikashutumiwa kwa mauaji ya halaiki. Kikosi hicho sasa kinadhibiti majimbo yote matano ya Darfur kati ya majimbo 18 ya Sudan, huku jeshi likidhibiti sehemu kubwa ya majimbo 13 yaliyosalia, yakiwemo Khartoum.
Eneo la Darfur linachukua takribani sehemu moja ya tano ya ardhi ya Sudan, lakini sehemu kubwa ya watu milioni 50 wa nchi hiyo wanaishi katika maeneo yanayodhibitiwa na jeshi.
Mgogoro nchini Sudan kati ya jeshi na RSF, ulioanza Aprili 2023, umeua angalau watu 40,000 na kuwahamisha milioni 12, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).
Comments
No comments Yet
Comment