Sport
Dollar
42,3350
0.2 %Euro
49,1712
0.05 %Gram Gold
5.547,4900
-0.07 %Quarter Gold
9.430,0100
0 %Silver
69,2000
0.51 %Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Michezo Sanaa na Utamaduni Gerson Msigwa amekemea taarifa zilizochapishwa na vyombo vya habari vya nje kuwa ziliendeshwa na nia mbaya ya kuichafua nchi.
Tanzania imeelezea ghadhabu yake kwa taarifa zilizochapishwa na baadhi ya vyombo vya habari vya nje kuwa zilifanywa kwa nia mbaya ya kutaka kuichafulia nchi jina.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Michezo Sanaa na Utamaduni Gerson Msigwa aliongeza kuwa taarifa hizo hazikuwa na haki na ni ukiukaji mkubwa.
‘‘Tunapoendelea kusubiri tume ikamilishe kazi yake, kumejitokeza wimbi kubwa la vyombo vya habari hususan vyombo vya habari vya nje kuchapisha na kutangaza taarifa ambazo ni za upande mmoja,’’ alisema Msigwa katika taarifa hiyo. ‘‘Na wakati mwengine kufanya upotoshaji wa taarifa wenye mlengo wa kuchochea chuki kwa Watanzania dhidi ya serikali, kuwagombanisha Watanzania wenyewe kwa wenyewe kutokana na tofauto zao za kisiasa kidini na kikanda,’’ aliongeza.
Msigwa alikuwa anazungumzia taarifa zilizochapishwa wiki hii na CNN pamoja na zingine zilizochapishwa na BBC na wengineo zikionyesha mauaji yanayodaiwa kufanywa wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29.
CNN iliripoti kuwa zaidi ya watu 2000 waliuawa kufuatia maandamano yaliyopinga matokeo ya uchaguzi mkuu na kuongeza kuwa vyombo vya uslama vilihusika katika kuficha mauaji hayo, japo walisema kuwa juhudi zao za kupata jibu la serikali hazikufua dafu.
Msigwa alikariri kuwa Rais Samia Suluhu Hassan, punde tu baada ya kuapishwa, ameunda tume maalum kuchunguza madai hayo na watakapo pokea ripoti ndipo watajua muelekeo wa kuchukua kama serikali.
Msigwa aliongeza kuwa Serikali nzima akiwemo Mama Samia Hassan, inasikitishwa na imeumizwa sana na matukio yale na madhara yake na akaviomba vyombo vya habari kushirikiana na serikali na kutoa taarifa zilizokamilika na za haki.
‘‘Serikali ipo tayari wakati wote kutoa ushirikiano kwa vyuombo vya habari vya ndani na vya nje ya nchi pale watakapotaka taarifa,’’ akisema Msigwa.
Pia Msigwa alitoa onyo kali kwa vyombo vya habari vya ndani na nje kutoingilia kazi ya tume iliyoundwa kuchunguza mauaji hayo.
‘‘Kama kuna chombo cha habari kina taarifa za uchunguzi kilioufanya kiwasilishe katika tume ili taarifa hizo zizingatiwe katika ripoti pale tume itakapokamilisha kazi yake,’’ alisema.
Rais Samia Suluhu Hassan alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa tarehe 29 Oktoba kwa asilimia 98 ya kura, lakini matokeo hayo yalisababisha maandamano makubwa ambayo vyombo vya usalama viliyakandamiza kwa ukali.
Baada ya kuapishwa, Rais Hassan alitangaza tume ya uchunguzi juu ya mauaji hayo, lakini upinzani ulisema haikuwa "huru wala isiyoegemea upendeleo".
Wanaharakati na upinzani wameitaka kuwa na maandamano ya amani tarehe 9 Desemba ili yaende sambamba na siku ya uhuru ya Tanzania.
Lakini polisi walisema mipango hiyo "inaonyesha uvunjaji wa amani na inakuza chuki ndani ya jamii, matendo yanayopingana na sheria".
Comments
No comments Yet
Comment