Hii ni baada ya Eisenkot, kiongozi wa chama cha Yashar kushindwa kufikia muafaka wa kuunda serikali na vyama vyengine na hatimae kumuita Netanyahu katika mazungumzo ya kuunda serikali ya pamoja

Eisenkot amtaka Netanyahu 'kuharakisha’ mazungumzo ya kuunda serikali ya pamoja

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amependekeza kuwepo kwa utaratibu wa kupokezana uwaziri mkuu na hasimu wake mkuu Gadi Eisenkot kwa kusema yuko tayari kumuachia aanze yeye. Waziri Mkuu wa zamani Yair Lapid ameliita pendekezo hilo “utapeli wa wazi unaofanywa na tapeli sugu”

Hii ni baada ya Eisenkot, kiongozi wa chama cha Yashar kushindwa kufikia muafaka wa kuunda serikali na vyama vyengine na hatimae kumuita Netanyahu katika mazungumzo ya kuunda serikali ya pamoja Jumamosi usiku, saa chache baada ya kupokea pendekezo la Netanyahu la kupokezana uwaziri mkuu.

Katika taarifa, Eisenkot amesema yeye pamoja na timu yake ya majadiliano walikuwa katika Hoteli ya Dan Accadia iliyopo Herzliya na walimualika Netanyahu na watu wake ili wajumuike katika “muongozo wa kweli na majadiliano ya sera,” limeripoti gazeti la Israeli daily Yedioth Ahronoth.

“Kama Likud iko tayari kwa umoja wa kweli, niko tayari kuangalia ukweli wa dhamira yake katika saa 24 zinazokuja,” amesema Eisenkot.

TRT Afrika — TRT Afrika

Picha: Reuters

#