Sport
Dollar
38,6415
0.03 %Euro
43,8951
-0.19 %Gram Gold
4.211,4800
-1.26 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameanza tena mazungumzo ya amani nchini Qatar, vyanzo vya habari vililiambia shirika la Reuters Jumanne.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameanza tena mazungumzo ya amani nchini Qatar, vyanzo vya habari vilisema siku ya Jumanne, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kumaliza mapigano mashariki wa DRC.
Pande zote mbili zilikutana Doha mwezi Aprili kujadili makubaliano ambayo yatamaliza kabisa vita mwaka huu ambavyo vimeua maelfu ya watu na kutia hofu ya kuwepo kwa vita zaidi katika kanda nzima.
Afisa mmoja ambaye anafahamu yanayojiri kwenye mazungumzo ya Doha ameiambia Reuters kuwa majadiliano ya sasa yalianza 3 Mei.
"Mazungumzo yanaendelea katika mazingira mazuri, na pande zote zimeeleza matumaini kuhusu majadiliano hayo," afisa huyo, ambaye ameomba jina lake lisitambulishwe, alisema.
Kipaumbele cha DRC 'ni amani'
Hata hivyo, vyanzo viwili vya upande wa waasi wa M23 vinasema kuwa wametuma wawakilishi wa ngazi ya chini ikilinganishwa na mazungumzo ya awali mwezi uliopita, na kulalamika kuwa ujumbe wa serikali haukupewa mamlaka ya kufanya maamuzi yoyote ukiwa Doha.
Pia walilalamika kuwa maafisa wa serikali hawajaonesha nia njema ya kuchukua hatua muafaka kama vile kuwaachilia huru washukiwa wa M23 wanaoshikiliwa na DRC.
Msemaji wa serikali hakujibu ombi la kutaka kuzungumzia suala hilo siku ya Jumanne. Chanzo kimoja kutoka kwa ofisi ya Rais wa Congo Felix Tshisekedi kimesema kipaumbele cha DRC ni amani na wako tayari kutoa msamaha kwa baadhi ya masuala.
Katika taarifa zilotolewa kwenye mazungumzo ya mwezi uliopita, pande zote ziliahidi kumaliza mapigano na kauli za uchochezi na kutoa wito kwa watu wa Congo kuunga mkono kusitishwa kwa mapigano na kusaidia kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya majadiliano.
Mapigano ya miongo kadhaa
Hata hivyo, wanaoshiriki katika mazungumzo hayo wanasema yanacheleweshwa na masuala madogo madogo ya kiufundi.
Mapigano mashariki mwa DRC yamekuwa yakiendelea. Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulika na misaada kwa watu ilisema siku ya Jumanne kuwa mapigano ya watu wenye silaha katika mkoa wa Kivu Kaskazini yamesababisha kuondolewa kwa watu wasiopungua 30,000 katika makazi yao tangu Ijumaa.
Qatar imekuwa ikihusika na mazungumzo ya kumaliza machafuko yanayoongezeka mashariki mwa DRC, ikiwa ni sehemu ya mapigano ambayo yameanza miongo kadhaa iliopita na yana chimbuko lake kwa mauaji ya kimbari ya Rwanda, tangu kuwaleta pamoja Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame mwezi Machi.
Umoja wa Mataifa na serikali za Magharibi zinasema Rwanda imetoa misaada ya silaha na wanajeshi kwa M23. Rwanda inakanusha kuwaunga mkono M23 na inasema jeshi limejitetea kuwa limekuwa likijilinda dhidi ya wanajeshi wa DRC na kundi la wapiganaji lililoundwa na waliohusika kwenye mauaji ya kimbari ya 1994.
Mazungumzo ya amani yanayoratibiwa na Marekani
Marekani pia inajaribu kuleta upatanishi kati ya DRC na Rwanda, ikihimiza makubaliano pamoja na miradi ya kiuchumi kukamilishwa kufikia mwezi Julai kwa mataifa yote mawili.
Massad Boulos, Mshauri mwandamizi wa masuala ya Afrika wa Rais wa Marekani Donald Trump, amesema kuwa mikataba ya mataifa yote mawili italeta uwekezaji wa mabilioni ya madola kutoka mataifa ya magharibi katika eneo ambalo lina utajiri wa madini muhimu zaidi.
Comments
No comments Yet
Comment