Sport
Dollar
40,1771
0.23 %Euro
47,0790
0.08 %Gram Gold
4.330,4600
1.09 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mamlaka ya afya inasema majimbo 17 kati ya 26 ya nchi hiyo yaliathiriwa, na idadi ya vifo imepanda kwa asilimia 2.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inapambana na kuenea kwa kasi kwa kipindupindu, hadi sasa maambukizi 1,601 yamethibitishwa kote nchini, mamlaka ya afya ilisema Alhamisi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kinshasa, Waziri wa Afya ya Umma Roger Kamba alisema nchi hiyo inakabiliwa na "mgogoro mkubwa wa kiafya" kutokana na majanga mengi na harakati nyingi za watu waliokimbia makazi yao, huku mikoa 17 kati ya 26 ikiathiriwa na ugonjwa wa kipindupindu.
Vituo vya afya 137 vimeathirika, jimbo la Tshopo ndilo lililoathirika zaidi baada ya kurekodi maambukizi 793, kulingana na waziri huyo, huku ugonjwa huo ukienea wakati pia kuna mzunguko wa ugonjwa wa mpox .
Alisema vitio 11 vya afya vinajiandaa kwa kutayarisha chanjo ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.
"Kwa sasa tunakabiliwa na magonjwa mawili ya milipuko: mpoks na kipindupindu. Kuhusu kipindupindu, tuko katika wiki ya 27 ya ufuatiliaji wa ugonjwa huu. Huku mikoa takriban 17 ambayo imeripoti maambukizi yaliothibitishwa au yanayoshukiwa, tuko katika hatua kali ya janga hilo, ambayo bado inaongezeka," alisema.
Kamba alisema katika mji mkuu Kinshasa pekee, maambukizi 130 huripotiwa kila wiki.
Kipindupindu, maambukizi ya bakteria, husababishwa na kula vyakula vichafu au kupitia maji machafu.
Akibainisha kuwa magonjwa mengi yanashughulikiwa na jamii, Kamba aliwashauri wananchi kuchukua hatua stahiki za usafi na kwenda kwenye vituo vya afya na kuepuka kujitibu kama wanakabiliwa na dalili zozote za kuhara na kutapika.
Mamlaka ya afya nchini Kongo ilitangaza mlipuko wa kipindupindu mwezi Mei mwaka huu, kufuatia uthibitisho wa kimaabara wa maambukizi katika mikoa mingi ya nchi hiyo.
Tangu kuzuka kwa kipindupindu, takriban maambukizi 33,000 yanayoshukiwa kuwa kipindupindu yameripotiwa na kiwango cha vifo cha karibu asilimia 2 ikiripotiwa nchini humo kutokana na mapungufu katika kuwafikia wagonjwa wa kipindupindu na matibabu ya mapema na ya kutosha, kulingana na wizara.
Waziri alisema upungufu wa dawa na mahitaji mengine hupunguza mwitikio wa kushughulikiwa ugonjwa wa kipindupindu, jambo ambalo linahitaji uelewa na ufuatiliaji zaidi.
Hata hivyo serikali, kwa msaada kutoka kwa Shirika la Afya Ulimwenguni na washirika wengine, ilianzisha mfumo wa kudhibiti madhara ili kuratibu mwitikio wa kitaifa kwa lengo la kupunguza maambukizi na kupunguza vifo vinavyotokana na kipindupindu.
Vitengo vya afya vinashughulikia maeneo yalioathirika ili kusaidia mamlaka za afya za mitaa kwa kutambua maambukizi, uchunguzi na usimamizi wa kimatibabu.
Comments
No comments Yet
Comment