Sport
Dollar
40,5964
0.02 %Euro
46,5288
0.41 %Gram Gold
4.296,0200
0.52 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi amesisitiza kuwa katika kipindi cha uchaguzi Tume itafanya kazi kwa karibu na taasisi na asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura.
Taasisi na asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu zimetakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya Tume.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele wakati akifungua mkutano wa Tume na taasisi na asasi hizo leo Julai 30, 2025 jijini Dar es Salaam.
”Nitoe rai kwenu haswa wale mliopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya Tume wakati wote wa utekelezaji wa zoezi hilo la kutoa elimu ya mpiga kura,” amesema Jaji Mwambegele.
Amesisitiza kuwa katika kipindi cha uchaguzi Tume itafanya kazi kwa karibu na taasisi na asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura.
Comments
No comments Yet
Comment