Dollar

43,4990

0.19 %

Euro

51,6240

-0.9 %

Gram Gold

6.788,9600

-9.85 %

Quarter Gold

12.225,8700

-6.97 %

Silver

116,5000

-28.39 %

Katika tukio hilo, ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania, ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kotoka jijini Accra, na kukaribishwa na salamu ya maji, maarufu kama ‘Water Salute’.

Air Tanzania yazindua safari za Ghana

Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) limezindua safari za ndege ya moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Accra nchini Ghana.

Kulingana na Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania, Makame Mbarawa, hatua hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON 2027), ambayo itaandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda.

Ili kurahisisha maandalizi ya AFCON 2027, Mbarawa alisema kuwa kutakuwa na ndege tatu za kila wiki, kati ya Dar es Salaam na Accra, ili kuimarisha uhusiano wa kiuchumi, na kurahisisha usafiri kati ya Afrika Mashariki na Magharibi.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu Mtendaji wa ATCL, Peter Ulanga, amesema hatua hiyo inaongeza idadi ya njia zake hadi 32, na kuimarisha ushindani wake katika soko la kimataifa.

Katika tukio hilo, ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania, ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kotoka jijini Accra, na kukaribishwa na salamu ya maji, maarufu kama ‘Water Salute’.

 

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#