Serikali ya Afrika Kusini yaanza hatua za kubatilisha maelfu ya viza zilizotolewa kinyume cha sheria huku ikipambana na rushwa ndani ya Idara ya Mambo ya Ndani.

Afrika Kusini yafuta zaidi ya viza 2,000 zilizopatikana kwa rushwa

Serikali ya Afrika Kusini imetangaza mpango wa kufuta zaidi ya viza 2,000 zinazodaiwa kutolewa kwa njia za rushwa na udanganyifu. Waziri wa Mambo ya Ndani, Leon Schreiber, amesema hatua hiyo inatokana na uchunguzi wa kina uliofichua mtandao wa maafisa waliokuwa wakitoa vibali kwa malipo haramu.

Uchunguzi wa Kitengo Maalum cha Uchunguzi (SIU) umebaini matumizi ya nyaraka feki, utoaji holela wa viza na vibali vya ukaazi, pamoja na malipo yaliyofanywa kupitia njia zisizo rasmi kama WhatsApp na pesa taslimu. Maafisa kadhaa wamefukuzwa kazi au kusimamishwa, huku mamia ya kesi za jinai zikiwasilishwa kwa mamlaka husika.

Rais Cyril Ramaphosa aliamuru uchunguzi wa utoaji wa viza kati ya 2004 na 2024, huku serikali sasa ikiahidi mageuzi ya kidigitali ili kuziba mianya ya rushwa na kurejesha imani ya umma katika mfumo wa uhamiaji.

Chanzo: TRT Afrika

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#