Marais wa nchi hizo mbili waamua kufufua haraka ushirikiano wa ulinzi wa mipaka na kupanua miradi ya maendeleo ya pamoja.

Algeria na Niger zakubaliana kuimarisha vita dhidi ya ugaidi Sahel

Marais wa Algeria na Niger, Abdelmadjid Tebboune na Abdourahamane Tiani, wamekubaliana kufufua mara moja mifumo ya pamoja ya kulinda mipaka na kupambana na ugaidi katika eneo la Sahel. Uamuzi huo umetangazwa baada ya ziara rasmi ya Tiani mjini Algiers, huku viongozi hao wakisisitiza kuwa usalama wa nchi zao unategemeana.

Pamoja na ushirikiano wa kiusalama, nchi hizo mbili zimekubaliana kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia, kufanya mikutano ya mara kwa mara ya ushirikiano, na kuharakisha miradi ya maendeleo ya pamoja. Hii inajumuisha kukamilisha barabara ya Trans-Sahara, mradi wa bomba la gesi la kuvuka jangwa, pamoja na miundombinu ya mawasiliano ya nyuzi za optic.

Katika sekta ya kiuchumi na kijamii, pande zote zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika nishati, biashara, ujasiriamali, teknolojia na huduma za kijamii. Pia wameahidi kurahisisha taratibu za biashara mipakani na kuanzisha masoko ya pamoja ili kuchochea maendeleo ya maeneo ya mpakani.

Ziara hiyo imehitimishwa kwa mwaliko wa Rais Tiani kwa mwenzake Tebboune kutembelea Niger, ambapo tarehe rasmi itatangazwa kupitia njia za kidiplomasia.

Chanzo:AA

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#