Sport
Dollar
41,4734
0.04 %Euro
48,8313
0.21 %Gram Gold
4.980,9200
0.04 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Rais wa Kenya William Ruto ametoa hotuba kali katika kikao cha 80 cha Umoja wa Mataifa jijini New York, akisema mabadiliko yanahitajika UN, IMF, Benki ya Dunia na taasisi zingine, kwa kuzingatia maslahi ya Afrika kwenye mabadiliko hayo.
Rais wa Kenya William Ruto ametoa hotuba kali katika kikao cha 80 cha Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York siku ya Jumatano.
Kiongozi huyo wa Kenya amegusia masuala mbalimbali katika hotuba yake akizungumzia hali mbaya kwa watu wa Gaza, vita vya Sudan, haja ya mabadiliko ya kitaasisi katika Umoja wa Mataifa na taasisi za kimataifa za fedha kama vile IMF na Benki ya Dunia, hali ya usalama Haiti, na taharuki za siasa kote duniani.
Hali ya Gaza
Ruto alieleza "wasiwasi mkubwa" wa Kenya kuhusu janga baya kwa watu wa Gaza na kutoa wito wa kusitishwa kabisa mapigano na kuheshimiwa kwa sheria ya kimataifa. "Kwa kupitia tu mchakato huo ndiyo dira ya kupatikana kwa suluhu ya mataifa mawili itafikiwa — ambapo Israel na Palestina watakuwa majirani, kwa amani na usalama."
IMF na taasisi kubwa za mikopo
Rais Ruto alishtumu taasisi za fedha za kimataifa kama vile IMF na Benki ya Dunia kwa "kutokuwa sawa" kwa Afrika. Alisema taasisi hizo zinaonekana kutoa fedha zaidi kwa mataifa tajiri huku "wakiadhibu" Afrika na riba kubwa, viwango vidogo vya mikopo, na masharti mengi sana.
Nafasi ya kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Rais Ruto alisisitiza kuwa Afrika inatakiwa kuwa na nafasi mbili za kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likuwa na uwezo wa kura ya turufu, na nafasi zingine mbili ambazo si za kudumu. Aliongeza kuwa mabadiliko ya Umoja wa Mataifa "siyo fadhila kwa Afrika", lakini ni lazima kwa shirika hilo kuendelea kuwa na maana. "Sehemu kubwa ya agenda ya Baraza la Usalama ni kuhusu Afrika… lakini bado ndiyo bara pekee ambalo halina nafasi ya kudumu kwenye Baraza hilo, ambapo maamuzi kuhusu hatma yetu yanafanywa. Dunia lazima ifahamu kuwa mabadiliko katika Baraza la Usalama siyo fadhila kwa Afrika; ni lazima kwa shirika hilo kuendelea kuwa na maana”
Umoja wa Mataifa kupoteza heshima
Rais Ruto pia alisema kuwa Umoja wa Mataifa, kama shirika, kwa sasa linakabiliwa "na changamoto kubwa kuhusu heshima yake," akisisitiza kuwa taasisi hiyo mara nyingi "inakuwa katika makabiliano na mataifa yenye uwezo mkubwa", kwa hiyo haifanyi kazi yake kama inavyotarajiwa.
Hali nchini Haiti
Rais Ruto anasema serikali yake, ambayo inaongoza ujumbe wa usalama katika nchi iliyoathiriwa na magenge ya wahalifu Haiti, bado ina dhamira ya kuendeleza ujumbe huo, lakini imekuwa ikikabiliwa na changamoto za ufadhili. "Ujumbe unaoongozwa na Kenya umekuwa ukifanya kazi katika mazingira magumu na changamoto nyingi. Hakuna ufadhili wa kutosha, hakuna vitendea kazi. Maafisa wetu wa polisi kwa ujasiri wao wamekuwa wakitekeleza majukumu yao bila kupewa uwezo kamili ambao hupewa ujumbe unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa."
Comments
No comments Yet
Comment