Sport
Dollar
43,3725
0.25 %Euro
51,3279
0.73 %Gram Gold
6.945,5100
1.57 %Quarter Gold
11.455,2500
2.32 %Silver
142,9700
6.92 %Mafuriko yameathiri maeneo ya Malawi, Msumbiji, Afrika Kusini, Tanzania, Zambia na Zimbabwe. WHO imeomba mahitaji ya dharura ya kibinadamu kama makazi, maji salama na upatikanaji wa huduma muhimu za afya.
Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeomba msaada wa haraka wa kibinadamu kwa nchi za Kusini mwa Afrika ili kusaidia kuzuia mlipuko wa magonjwa yanayosambazwa kupitia maji machafu.
Magonjwa yanayoenezwa na maji, hasa kuhara na kipindupindu ni tishio kubwa katika maeneo yanayohifadhi watu waliohamishwa na mafuriko kutokana na msongamano wa watu, huduma duni za usafi binafsi na huduma za usafi wa mazingira pamoja na uhaba wa maji salama.
Kulingana na Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika, Dk Mohamed Janabi, kuhama kwa watu wengi na miundombinu duni ya maji, usafi na uchafuzi wa mazingira, husababisha hatari ya maambukizo ya haraka ya magonjwa ya mfumo wa kupumua ,nimonia na magonjwa ya ngozi.
‘’Lengo letu la haraka ni kuzuia milipuko ya magonjwa, kudumisha huduma muhimu za afya, kuokoa maisha na kulinda jamii zilizo hatarini zaidi,” alisema Dk Janabi.
Mvua kubwa na mafuriko tangu katikati ya Desemba 2025 yameathiri karibu watu milioni 1.3 kusini mwa Afrika, kuharibu nyumba na miundombinu muhimu na kutatiza upatikanaji wa huduma za afya, na kuongeza hatari ya magonjwa ya maji na mbu.
Takriban nusu ya watu walioathirika wako Msumbiji, kulingana na tathmini za awali za Shirika la Afya Duniani (WHO). Mafuriko hayo pia yameathiri maeneo ya Malawi, Afrika Kusini, Tanzania, Zambia na Zimbabwe. Mahitaji ya dharura ya kibinadamu ni pamoja na makazi, maji salama na upatikanaji wa huduma muhimu za afya.
WHO hata hivyo imesema jumla ya mamabukizi 4385 yimeripotiwa kufikia Januari 2026 kutoka nchi 10 ikilinganishwa na zaidi ya kesi 20,000 zilizoripotiwa kutoka nchi 14 Januari 2025.
Comments
No comments Yet
Comment