Sport
Dollar
38,8018
0.05 %Euro
43,0975
0.09 %Gram Gold
4.035,7900
0.01 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Wanadiplomasia mkubwa wa Uturuki Hakan Fidan ameelezea alivyosalimika jaribio la kuuawa kupitia sumu ya zebaki na aseniki.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan, amesema amekuwa akilengwa katika jaribio la kuuawa ambapo sumu mbaya za chuma zilitumika miaka mine na mitano iliyopita.
Akizungumza katika mahojiano na 24 TV, Fidan amesema kiwango kikubwa cha zebaki na aseniki kimetumika dhidi yake.
“Haya yaligundulika katika vipimo,” ameongeza, na kusema kuwa alipewa sumu na hiyo ilikuwa ni jaribio dhidi ya maisha yake.
Fidan, ambae awali aliongoza kitengo cha Uturuki cha Taifa cha Intelijensia (MIT), amesema amekuwa akilengwa na makundi ya kigaidi tangu aingie katika kitengo hicho.
Pia amewalaumu wapinzani wakuu wa nchi, kwa kutumia taarifa zinazodaiwa kutolewa na makundi ya kigaidi na mitandao ya kihalifu kusukuma ajenda za kisiasa.
“Hii ni njia ya hatari,” amesema Fidan. “Mbali na mauaji ya wahusika, pia tumelengwa waziwazi. Nilipewa sumu.”
Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu ni lini au wapi ilitokea.
Fidan ameshikilia nyadhifa mbalimbali mambo ya nje na usalama ndani ya serikali ya Uturuki.
Comments
No comments Yet
Comment