Sport
Dollar
38,8010
0.04 %Euro
43,1228
0.14 %Gram Gold
4.040,8500
0.14 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Putin amezipigia simu mamlaka za Kiev ili kuanza mazungumzo ya amani Alhamisi, Mei 15, jijini Istanbul.
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonyesha utayari kwa Ukraine Jumapili wa kuanza mazungumzo ya amani jijini Istanbul, kuanzia Mei 15.
Putin amesema katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Moscow kwamba Jumatatu atafanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na kuomba jukwaa la mazungumzo ili kujadili njia ya amani na Ukraine.
“Urusi iko tayari kwa majadiliano bila masharti. Kuna vita vinaendelea sasa hivi, na tunapendekeza kurudi katika majadiliano. Wale wanaotaka amani watalikubali hili,” amesema.
Rais ameongeza kusema kuwa makubaliano mapya ya usitishaji wa mapigano yanaweza kujadiliwa Istanbul.
“Mapendelezo yetu yapo mezani, na imebaki kwa mamlaka ya Ukraine na wasimamizi wake,” amesema.
Urusi na Ukraine zilifanya mazungumzo Istanbul Machi 2022 na kukubaliana kuhusu rasimu ya makubaliano ya amani.
Comments
No comments Yet
Comment