Tokyo: 05:18 PM
Londra: 08:18 AM
New York: 03:18 AM
İstanbul: 11:18 AM

Dollar

39,1011

0.04 %

Euro

44,4609

0.52 %

Gram Gold

4.202,2600

1.92 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rumeysa Ozturk, aliyeshikiliwa nchini Marekani kwa kuonyesha kuiunga mkono Palestina, amewashukuru walioonyesha mshikamano baada ya kuachiliwa katika kituo cha Louisiana, vyombo vya habari vimeripoti

Mwanafunzi wa Kituruki aliyeachiliwa Marekani awashukuru waliomuunga mkono

Mwanafunzi wa Kituruki wa shahada ya uzamivu amewashukuru wale waliomuunga mkono katika kipindi chote alichokuwa ameshikiliwa nchini Marekani kwa kuiunga mkono Palestina, vyombo vya habari vimeripoti siku ya Ijumaa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la CPS, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tufts Rumeysa Ozturk ameongea kwa ufupi na vyombo vya habari baada kuondoka kituo cha uhamiaji Louisiana alipokuwa amezuiliwa tangu mwishoni mwa mwezi Machi.

“Asanteni sana kwa kuniunga mkono na upendo,” aliwaambia wafuasi. “Nimechoka kidogo kwa hiyo nitapumzika kidogo lakini nashukuru sana kwa kuwa hapa.”

Picha za kuachiwa kwake zinaonyesha kundi la wanaomuunga mkono likisherehekea wakati Ozturk akitoka katika kituo hicho.

Ozturk alikamatwa na maafisa sita ambao hawakuvaa sare za kazini Machi 25 Massachusetts wakati akielekea katika chakula cha usiku mwezi mtukufu wa Waislamu wa Ramadhani pamoja na rafiki zake.

Baadae Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alitangaza kufutwa kwa viza yake ya mwanafunzi na kwamba atarudishwa nchini mwake.

Rubio amewatuhumu zaidi ya wanafunzi 300 wa kigeni kwa '“kuiunga mkono Hamas.” Lakini amri ilitolewa ya kuwakamata na kuwarudisha bila kuwapa nafasi ya kujitetea.

Wakosoaji wanasema, kuwarudisha kwa sababu ya kutoa maoni yao kunakiuka haki yao ya kikatiba ya kujieleza-haki ambayo anapewa kila mtu nchini Marekani, raia na wasiokuwa raia.

Hakimu katika mahakama ya Marekani, Denise Casper, alizuia mchakato wa kurudishwa kwa Ozturk, na hakimu mwengine, William Sessions wa Mahakama ya Wilaya nchini Marekani katika eneo la Vermont, alitoa amri ya kuachiwa kwa dhamana.

Chuo Kikuu cha Tufts kimetaka kuachiliwa kwa Ozturk, na katika taarifa yake kwa mahakama, Rais wa Chuo Sunil Kumar amesema kushikiliwa “kumezorotesha jamii ya kimataifa” na kuibua wasiwasi mkubwa kuhusu usalama chuoni hapo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#