Dollar

38,8047

0.05 %

Euro

43,1940

0.25 %

Gram Gold

4.025,8100

-0.24 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

"Nadhani kutapatikana tija kutoka kwenye mkutano huo," amesema rais wa Marekani kuhusu mazungumzo ya amani ya Alhamisi jijini Istanbul.

Mazungumzo ya Urusi na Ukraine nchini Uturuki 'ni ya muhimu sana' — Trump


Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza umuhimu wa mazungumzo ya wiki hii ya amani kati ya Urusi na Ukraine yatakayofanyika Uturuki, akiongeza kuwa anadhani "kutapatikana tija kutoka” kwenye mazungumzo hayo.

"Mkutano wa Alhamisi na Urusi na Ukraine ni muhimu sana," Trump amewaambia waandishi wa habari. "Nilisisitiza sana kuwa lazima mkutano huo ufanyike."

Alieleza matumaini yake kuhusu matokeo ya mazungumzo hayo’, akisema: "nadhani kutapatikana tija kutoka kwenye mkutano huo."

"Usifanye mzaha" na mkutano wa Alhamisi, Trump alieleza, akimpongeza Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kama "mwenyeji mzuri."

"Nilikuwa nafkiria kuhusu kusafiri kwenda huko kwa ajili ya huo mkutano", alisema, akiongeza kuwa huenda akasafiri kwenda Uturuki "ikiwa nadhani mambo yatakuwa mazuri."

Akieleza kuhusu “ukatili” wa vifo vya watu uliotokea katika mapigano hayo, aliueleza kama "mbinu mpya za kivita.”

Trump ametoa wito wa kumalizika "kwa umwagikaji damu" Ukraine, akisema kuwa watu "wanauawa katika viwango ambavyo hatujawahi kuona tangu Vita vya Pili vya Dunia."

Mazungumzo haya ya amani yanatarajiwa kufanyika jijini Istanbul, Uturuki, baada ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kuonesha kukubali mapendekezo ya Urusi ya kuanza tena mazungumzo baada ya kusitishwa kwa muda mrefu.

Erdogan amefurahishwa na hatua ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kuunga mkono kuanzishwa tena kwa mchakato wa amani kutoka pale ulipositishwa jijini Istanbul Machi 2022, akisisitiza kuhusu dhamira ya Uturuki katika juhudi za amani.​​​​​​​

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#