Sport
Dollar
40,6865
0.18 %Euro
47,4766
-0.04 %Gram Gold
4.430,6400
-0.09 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Waziri Mkuu wa Kenya Musalia Mudavadi amethibitisha haya wakati muswada unaopendekezwa katika Seneti ya Marekani ukitishia kufuta hadhi ya nchi hiyo isiyo ya NATO (MNNA) kuhusu uhusiano wake wa kibiashara na Iran na Urusi.
Serikali ya Kenya imepuuza tishio kwamba Marekani huenda ikafuta uhusiano wake wa Karibu na nchi hiyo.
Hio ni kufuatia ripoti kuwa seneta mmoj wa Marekani amependekeza Marekani ichunguze na kutathmini uhusiano wake na Kenya.
Waziri Mkuu wa Kenya Musalia Mudavadi amethibitisha haya wakati muswada unaopendekezwa katika Seneti ya Marekani ukitishia kufuta hadhi ya nchi hiyo isiyo ya NATO (MNNA) kufuatia uhusiano wake wa kibiashara na Iran na Urusi.
Akizungumza na wabunge siku ya Alhamisi, Musalia alipuuza madai kwamba uhusiano wa kidiplomasia wa Kenya na Tehran na Moscow ulikuwa wa hatari.
“Tuna uhusiano na Iran kwa sababu ni wanunuzi wakubwa wa chai yetu. Kama serikali tuna jukumu la kutafuta soko kwa wakulima wetu wa chai, lazima tuuze kahawa, na maua yetu. kwa hiyo lazima kutafuta soko,” Mudavadi amesema.
Alisisitiza kuwa taifa lilikuwa linatumia tu haki yake kuu ya kutafuta fursa za kiuchumi kwa wakulima na wafanyabiashara wake.
Comments
No comments Yet
Comment