Sport
Dollar
40,2622
0.13 %Euro
46,7980
0.14 %Gram Gold
4.311,4400
0.33 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Watu wenye silaha wamewaua wasiopungua 27 katika jimbo la kaskazini kati mwa Nigeria la Plateau, katika machafuko ya hivi karibuni katika eneo lisilo na usalama wa kutosha.
Watu wasiopungua 27 wameuawa na waliokuwa na silaha kaskazini kati mwa jimbo la Nigeria la Plateau, katika machafuko ya hivi karibuni katika eneo ambalo halina usalama wa kutosha, vyanzo vya maeneo hayo vimeiambia AFP Jumanne.
Jimbo la Plateau state, kama ilivyo maeneo mengine nchini Nigeria katika sehemu hiyo, limekuwa likikabiliwa na mapigano kati ya wakulima na wafugaji wakigombania ardhi na raslimali asilia, pamoja na vurugu zinazozushwa na wahalifu.
Mkazi mmoja Haggai Gankis ameiambia AFP kuwa washambuliaji walienda kwenye eneo la Jebu-Rahoss, siku ya Jumatatu jioni, wakiwa na bunduki na mapanga.
Alilaumu mashambulizi hayo kwa wafugaji. Mkazi mwingine, Chuwang David, alilaumu makundi ya wahalifu.
'Walipiga risasi watu wengi'
"Tulikuwa tumelala usiku, tukaskia milio ya risasi, washambuliaji walipiga risasi watu wengi sana na pia walitumia mapanga," David alisema.
Da Chomo Moses, mkazi mwingine, pia alitoa idadi kama hiyo na kusema kuwa alipoteza wanafamilia watatu.
"Watu ishirini na saba ambao hawakuwa na hatia waliuawa kwa risasi," alisema Gankis, akiongeza kuwa wengi wao walikuwa wanawake.
Mwenyekiti wa serikali za mitaa Sati Bature Shuwa alithibitisha kuhusu shambulizi hilo kwa AFP, lakini hakutoa idadi.
Watu kadhaa wapelekwa hospitali
Wakazi wanasema kuna idadi isiyojulikana ya watu ambao walipelekwa hospitali.
Kwa miaka kadhaa, mashambulizi ya watu wenye silaha yameongezeka vijijini kaskazini magharibi na katikati mwa Nigeria.
Hofu ya kisiasa na kiuchumi kati ya wazawa na wale wanaoonekana wa kuja imeongezeka na kusababisha tofauti kubwa katika miongo ya hivi karibuni.
Wafugaji pia wanasema wanashambuliwa
Mashambulizi kote katika jimbo la Plateau na jimbo la jirani la Benue yamesababisha vifo vya watu zaidi 150 mwezi Aprili peke yake.
Wakati mauaji yaliolaumiwa kwa wafugaji yamesababisha taharuki nchi nzima, wafugaji nao wanasema pia wao wanashambuliwa.
Machafuko mengi katika jimbo la Plateau yanatokea maeneo ambayo kuna polisi wachache.
Comments
No comments Yet
Comment