Sport
Dollar
40,2611
0.13 %Euro
46,8110
0.22 %Gram Gold
4.311,5500
0.33 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Rais wa zamani wa Nigeria Muhammadu Buhari amezikwa katika eneo la nyumbani kwake katika jimbo la kaskazini mashariki la Katsina.
Rais wa zamani wa Nigeria Muhammadu Buhari amezikwa nyumbani kwake katika jimbo la kaskazini magharibi la Katsina siku ya Jumanne, huku viongozi kadhaa wakihudhuria, na kukiwa na ulinzi mkali.
Maelfu ya raia wa Nigeria walikusanyika kwa swala ya pamoja katika mji wa Daura kabla kiongozi huyo wa zamani kuzikwa katika mazishi ya faragha kwenye eneo la nyumbani kwake.
Buhari, ambaye alifariki akiwa na umri wa 82 katika hospitali moja jijini London siku ya Jumapili, aliongoza Nigeria kwanza akiwa kiongozi wa nchi wa kijeshi katika miaka ya themanini na baadaye akachaguliwa rais kwa njia ya demokrasia, na kuhudumu kwa mihula miwili kuanzia 2015 hadi 2023.
Rais wa Nigeria Bola Tinubu, mtu tajiri zaidi barani Afrika Aliko Dangote, rais wa Guinea-Bissau na waziri mkuu wa Niger, pamoja na rais wa zamani wa Niger Mahamadou Issoufou wote walihudhuria, vyombo vya habari vya nchini humo viliripoti.
Maafisa wengi wa usalama
Kuwepo kwa Waziri Mkuu wa Niger Ali Lamine Zeine kumekuja baada ya uhusiano wa nchi yake wa kidiplomasia na Nigeria kuharibika kufuatia mapinduzi ya Niger 2023 ambapo serikali ya kidemokrasia ya Rais Mohamed Bazoum ilipinduliwa.
Wakati mwili wa Buhari ulipokuwa katika safari yake kutoka England hadi Daura, mji ulioko chini ya kilomita 20 kutoka mpaka wa Niger, kulikuwa na idadi kubwa ya maafisa wa usalama polisi, wanajeshi na maaskari kanzu walipelekwa katika mji huo.
Kwa miaka mingi Nigeria, hasa kusini mwa nchi, imekuwa ikishambuliwa na magaidi na magenge ya wahalifu.
Buhari aliweka historia 2015 kwa kuwa mgombea wa kwanza wa upinzani kumshinda rais aliyekuwepo madarakani katika uchaguzi.
Heshima za kijeshi
Picha kutoka eneo hilo la nyumbani kwake zilionesha bendi ya kijeshi ikitoa heshima za mwisho kwa Buhari, ambaye jeneza lake lilikuwa limefunikwa na bendera ya taifa la Nigeria, huku wanajeshi wakipiga saluti.
Vijana walipanda juu ya miti ili kuona yanayoendelea kwenye mazishi hayo.
Ulinzi ulikuwa mkali huku baadhi ya jamaa zake Buhari wakifungiwa nje ya eneo hilo Jumanne mchana.
Comments
No comments Yet
Comment