Dollar

41,9489

-0.15 %

Euro

48,8502

-0.23 %

Gram Gold

5.540,5600

-0.59 %

Quarter Gold

9.664,4100

-0.12 %

Silver

65,5800

-0.8 %

“Kwa zaidi ya mwezi mmoja, hali ya kibinadamu mjini El-Fasher imezidi kuwa mbaya sana,” Kundi la Madaktari la Sudan limesema katika taarifa.

Watoto watatu hufa kila siku El-Fasher nchini Sudan kutokana na utapiamlo: Ripoti

Takriban watoto watatu wanakufa kila siku katika mji wa El-Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan, kutokana na utapiamlo na magonjwa, kulingana na taarifa iliyotolewa na Kundi la Madaktari la Sudan siku ya Ijumaa.

“Kwa zaidi ya mwezi mmoja, hali ya kibinadamu mjini El-Fasher imezidi kuwa mbaya sana, huku idadi ya vifo vya watoto ikiendelea kuongezeka kutokana na uhaba wa chakula na kuongezeka kwa visa vya utapiamlo, bila ya kuwa na dalili za kufunguliwa kwa njia yoyote ya misaada ya kibinadamu ambayo ingeweza kuokoa maelfu ya watoto,” ilisema taarifa hiyo.

Kundi hilo limesema “tunafuatilia kwa wasiwasi mkubwa hali hiyo ya kusikitisha kupitia wafanyakazi wetu huko El-Fasher. Tunwathibitishia jumuiya ya kimataifa kwamba hali ya kibinadamu imezidi kuzoroteka kutokana na uhaba wa chakula na dawa unaosababishwa na kizuizi kinachoendelea,” iliongeza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliongeza: “Kila siku inayopita, tunapoteza takriban watoto watatu kutokana na utapiamlo, magonjwa, na uhaba mkubwa wa rasilimali za matibabu na kibinadamu.”

Alhamisi, mashirika manne ya Umoja wa Mataifa -- Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, UNICEF, Mpango wa Chakula wa Dunia, na shirika la wakimbizi la UN -- yalieleza katika taarifa ya pamoja kuwa raia 260,000, ikiwa ni pamoja na watoto 130,000, wamekwama El-Fasher, bila chakula, maji, na huduma za afya.

Takriban watoto 239 wamekufa kwa njaa kutokana na kuzingirwa kwa eneo la El-Fasher na wapiganaji wa RSF, tume ya “El-Fasher Resistance Coordination” ilisema Jumatano, bila kutaja kipindi cha wakati wa vifo hivyo.

RSF, kikosi cha wapiganaji, kimezingira El-Fasher tangu Mei 10, 2024, huku jeshi la Sudan likijaribu kuvunja kizuizi cha mji huo, ambacho ni kituo cha shughuli za kibinadamu kwa mikoa mitano ya Darfur.

Jeshi la Sudan na RSF wamekuwa wakipigana vita tangu Aprili 2023 ambavyo vimewaua zaidi ya watu 20,000 na kuwalazimisha watu 14 milioni kuhama makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa na mamlaka za eneo hilo.

Hata hivyo, utafiti kutoka vyuo vikuu vya Marekani unakadiria idadi ya vifo kuwa karibu 130,000.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#