Sport
Dollar
41,9489
-0.15 %Euro
48,8502
-0.23 %Gram Gold
5.540,5600
-0.59 %Quarter Gold
9.664,4100
-0.12 %Silver
65,5800
-0.8 %Mabadiliko hayo ni ya "kuimarisha usalama wa taifa", kulingana na msemaji wa Rais, na pia yanakuja siku chache baada ya kitengo cha ulinzo nchini humo kukana madai ya njama ya mapinduzi.
Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, ameteua maafisa wapya wakuu wa kijeshi katika mabadiliko makubwa ya uongozi wa jeshi la taifa, Ofisi ya Rais imesema Ijumaa, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha usalama wa taifa.
Mabadiliko haya yanakuja wakati changamoto za usalama zikiendelea kutatiza Nigeria, ikiwa ni pamoja na mapigano ya wanamgambo katika eneo la kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.
Jenerali Olufemi Oluyede amepewa wadhifa wa Kamanda Mkuu wa Ulinzi, akichukua nafasi ya Jenerali Christopher Musa, aliyeteuliwa zaidi ya miaka miwili iliyopita baada ya Tinubu kuingia madarakani.
Major-Jenerali W. Shaibu amepewa wadhifa wa Kiongozi wa Jeshi , wakati Air Vice Marshal S.K. Aneke na Rear Admiral I. Abbas wamepewa vyeo vya Wakuu wa Jeshi la Anga na Majini.
Major-Jenerali E.A.P. Undiendeye ameendelea kushikilia wadhifa wake kama Kiongozi wa Upelelezi wa Ulinzi.
“Mabadiliko hayo yataanza kutekelezwa mara moja,” Ofisi ya Rais imesema katika taarifa.
Comments
No comments Yet
Comment