Dollar

38,5849

0.04 %

Euro

43,8558

0.48 %

Gram Gold

4.114,9900

2.39 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rais William Ruto alirushiwa kiatu alipokuwa anawahutubia wakazi wa eneo la Kehancha, kaunti ya Migor siku ya Jumapili.

Watatu mbaroni baada ya Rais Ruto kurushiwa kiatu

Polisi nchini Kenya wanawahoji watu watatu baada ya mtu mmoja kumrushia kiatu Rais William Ruto katika eneo la Kuria Magharibi, Kaunti ya Migori.

Kisa hicho kilitokea huku Rais Ruto akihutubia wakazi wa eneo la Kehancha siku ya Jumapili.

Polisi walisema uchunguzi unaendelea na kwamba washukiwa zaidi wanafuatiliwa.

Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen alisema watatu hao wanachukuliwa kama sehemu ya uchunguzi mpana kuhusu iwapo kitendo hicho kilikuwa ni jaribio la makusudi la kuvunja usalama wa rais.

Video fupi ya tukio hilo inaonyesha kiatu kikitua kwenye mkono wa kushoto wa Rais Ruto, alipokuwa akitoa hotuba yake.

Kikosi cha usalama cha rais kilichukua hatua ya kumlinda mkuu huyo wa nchi, ingawa kiatu kilikuwa tayari kimempiga mkononi.

Ziara ya maendeleo Rais

Ruto alianza ziara yake ya siku tatu ya maendeleo katika kaunti ya Migori Magharibi mwa Kenya siku ya Jumapili. Migori iko zaidi ya kilomita 370 magharibi mwa mji mkuu wa Kenya Nairobi.

Kaunti ya Migori kwa kiasi kikubwa inaungwa mkono na upinzani, ambao unaongozwa na mwanasiasa mkongwe Raila Odinga, ambaye alishindana na Ruto bila mafanikio katika uchaguzi wa urais wa Agosti 2022 nchini Kenya.

Rais Ruto na Odinga, ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu wa Kenya kuanzia 2008 hadi 2013, wameingia katika mkataba wa ushirikiano.

Utawala wa Rais Ruto, ambao unahudumu kwa muhula wake wa kwanza wa miaka mitano, mara kadhaa umekabiliwa na chuki kutoka kwa Wakenya, ambao wanakashifu ushuru mkubwa na gharama ya juu ya maisha tangu kuingia madarakani Septemba 2022.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#