Dollar

43,2789

0.22 %

Euro

50,2002

-0.1 %

Gram Gold

6.375,3800

-0.3 %

Quarter Gold

10.664,4800

0.75 %

Silver

124,3300

-2.65 %

Imamu Abubakar Abdullahi alipata umaarufu kwa kukataa kuwakabidhi watu waliokimbilia msikitini kwake, licha ya kutishiwa maisha yake.

Wanigeria waomboleza kifo cha Imamu aliyewaokoa Wakristo wakati wa shambulio

Salamu za rambirambi zimetolewa kwa Imamu wa msikiti Nigeria, Abubakar Abdullahi, aliyepata umaarufu duniani mwaka 2018 alipofungua msikiti na nyumba yake ili kuwahifadhi na kuwalinda takribani Wakristo mia tatu wakati wa shambulio la majambazi wenye silaha.

Abdullahi alifariki dunia siku ya Alhamisi katika hospitali ambako alikuwa amelazwa baada ya kugunduliwa kuwa na tatizo la moyo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia yake iliyonukuliwa na vyombo vya habari vya Nigeria. Alikuwa na umri wa miaka 92.

Mashambulizi dhidi ya vijiji katika jimbo la Plateau yalitokea wakati wa wa mvutano wa kijamii, ambapo jimbo hilo lililoko kaskazini-kati mwa Nigeria lilishuhudia migogoro ya mara kwa mara ya kikabila na kidini iliyosababisha vifo vya maelfu ya watu.

Mwanazuoni huyo wa Kiislamu ambaye sasa ni marehemu, alikataa kwa uthabiti kuwakabidhi watu waliokuwa wamekimbilia msikitini wake, licha ya vitisho dhidi ya maisha yake kutoka kwa washambuliaji.

Tuzo kutoka serikali ya Marekani

Ujasiri wake ulimletea sifa na kutambuliwa kwa kiwango kikubwa, ikiwemo Tuzo ya Kimataifa ya Uhuru wa Kidini ya mwaka 2019 kutoka kwa serikali ya Marekani.

Serikali ya Nigeria pia ilimtunuku heshima ya kitaifa mwaka 2022.

Kiongozi wa upinzani nchini Nigeria, Atiku Abubakar, alimwelezea marehemu imamu kama “mzalendo wa kipekee na mfano wa huruma.”

“Kitendo chake cha ujasiri hakikuokoa tu mamia ya maisha, bali pia kilisimama kama ushahidi wenye nguvu kwamba amani, uelewano, na udugu ndiyo misingi imara zaidi ya umoja wa kitaifa,” alisema katika chapisho kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii la X.

Gavana wa jimbo la Plateau, Caleb Mutfwang, alisema kifo cha Imamu Abubakar ni “hasara kubwa sana kwa familia yake ya karibu na jamii yake.”

Katika taarifa yake, gavana huyo alimsifu Abubakar kwa “dhamira yake isiyotetereka ya kudumisha amani, umoja, na kuwalinda walio hatarini, hasa wanawake na watoto.”

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#