Dollar

43,2789

0.22 %

Euro

50,2002

-0.1 %

Gram Gold

6.375,3800

-0.3 %

Quarter Gold

10.664,4800

0.75 %

Silver

124,3300

-2.65 %

Takriban watu kumi wameuawa katika ghasia zilizotokea usiku katikati mwa Uganda, polisi walisema siky ya Ijumaa, kufuatia uchaguzi ambao unaonekana kumpa Rais mkongwe Yoweri Museveni ushindi.

Takriban watu kumi wauawa Uganda, kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi yalionyesha Museveni akiwa amepata zaidi ya asilimia 75 ya kura katika uchaguzi wa urais uliofanyika siku ya Alhamisi. Mpinzani wake mkuu, mwanamuziki maarufu Bobi Wine, alipata takribani asilimia 21, huku kura zilizobaki zikigawanywa miongoni mwa wagombea wengine sita.

Baada ya kampeni iliyokumbwa na mapigano katika mikutano ya upinzani na kile Umoja wa Mataifa ulieleza kuwa ni ukandamizaji na vitisho vilivyoenea, upigaji kura ulifanyika kwa amani siku ya Alhamisi.

Hata hivyo, ghasia zilianza usiku katika mji wa Butambala, takribani kilomita 55 kusini-magharibi mwa mji mkuu Kampala, kulingana na msemaji wa polisi na mbunge wa eneo hilo, ambao walitoa maelezo yanayokinzana kuhusu tukio hilo.

Ghasia na mauaji

Msemaji wa polisi wa eneo hilo, Lydia Tumushabe, alisema kuwa wahuni wa upinzani waliokuwa na mapanga, waliodaiwa kutumwa na mbunge wa eneo hilo Muwanga Kivumbi, walivamia kituo cha polisi na kituo cha kuhesabia kura.

“Vyombo vya usalama vilijilinda kwa sababu watu hawa walikuja kwa idadi kubwa. Polisi walifyatua risasi kwa ajili ya kujilinda,” alisema akizungumza na shirika la habari la Reuters, na kuongeza kuwa watu 25 walikamatwa.

Hata hivyo, Kivumbi aliieleza shirika hilo la habari kuwa watu hao waliuawa saa tisa usiku (saa sita usiku kwa saa za GMT) ndani ya nyumba yake, walipokuwa wakingojea matokeo ya uchaguzi wa ubunge katika jimbo lake.

“Waliua watu 10 ndani ya nyumba yangu,” alisema. “Kulikuwa na watu ndani ya gereji wakisubiri matokeo ili kusherehekea ushindi wangu.”

“Walivunja mlango wa mbele na kuanza kufyatua risasi ndani ya gereji. Ilikuwa mauaji ya kikatili.”

Alisema kuwa vikosi vya usalama vilikuwa tayari vimetawanya umati nje ya nyumba, lakini alipinga madai ya polisi kuwa vifo vilitokea wakati wa mapambano kati ya pande hizo mbili.

Tumushabe, msemaji wa polisi, alisema hakuwa na taarifa kuhusu tukio lolote lililotokea katika nyumba ya Kivumbi, ambayo alisema iko karibu na kituo cha polisi.

Reuters haikuweza kuthibitisha madai ya pande hizo mbili na mazingira halisi ya ghasia hizo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#