Dollar

43,4775

-0.04 %

Euro

51,3687

-0.46 %

Gram Gold

6.544,4600

-3.6 %

Quarter Gold

11.661,9400

-2.17 %

Silver

110,1500

-5.45 %

Jeshi linasema lilifanya operesheni katika msitu wa Sambisa jimbo la Borno

Wanajeshi wa Nigeria wamuua kamanda wa Boko Haram, wapiganaji 10 kaskazini mashariki mwa nchi

Jeshi la Nigeria limesema siku ya Jumapili nkuwa vikosi vyake vilimuua kamanda wa Boko Haram na wapiganaji wengine 10 wa kundi hilo la kigaidi wakati wa operesheni kaskazini mashariki mwa nchi.

Katika taarifa, jeshi linasema kuwa vikosi vyake ilifanya operesheni hiyo katika msitu wa Sambisa ulioko jimbo la Borno.

Kamanda huyo aliyeuawa ametajwa kuwa ni Abu Khalid, ambaye alikuwa wa pili kwenye uongozi wa Boko Haram msitu wa Sambisa. Alielezewa kuwa mtu muhimu ndani ya kundi hilo la kigaidi ambaye alikuwa na majukumu ya kuratibu operesheni na mipango msitu wa Sambisa.

Hakuna aliyesemekana kuuawa upande wa wanajeshi wa Nigeria, taarifa hiyo iliongeza, kuwa operesheni dhidi ya ugaidi zinaendelea katika maeneo ya misitu kote kaskazini mashariki.

Boko Haram imekuwa ikifanya mashambulizi Nigeria tangu mwanzoni mwa miaka 2000, huku maelfu ya watu wakiuawa tangu 2009.

Tangu 2015, kundi hilo limekuwa likifanya mashambulizi katika nchi jirani za Cameroon, Chad na Niger, na kuwaua watu wasiopungua 2,000 kote katika eneo la Ziwa Chad, kulingana na mamlaka.

Maelfu ya watu pia wamelazimika kuondoka katika makazi yao kutokana na mashambulizi ya kigaidi na mapigano yanayoendelea katika eneo hilo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#