Sport
Dollar
41,3970
0.08 %Euro
48,6749
-0.05 %Gram Gold
4.844,4300
0.33 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Ujenzi wa Hospitali ya Sogoo katika kaunti ya Narok haukumfurahisha Rais wa Kenya William Ruto alipozuru eneo hilo Mei mwaka huu, jambo lililomfanya kuagiza wanajeshi kuingilia kati.
Rais William Ruto ametuma Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) kusimamia ujenzi wa vituo vya afya zaidi ya 75 kote nchini katika juhudi za kuhakikisha unakamilika haraka.
Akizungumza katika Kaunti ya Narok wakati wa uzinduzi wa hospitali ya Sogoo Level 4, Waziri wa Ulinzi Patrick Mariru alifichua kuwa Hospitali hiyo yenye mamlaka kamili itakamilika baada ya miezi 11.
Ujenzi wa Hospitali ya Sogoo haukumfurahisha Rais Ruto alipozuru eneo hilo Mei mwaka huu, jambo lililomfanya kuagiza KDF kuiboresha.
"Jeshi litamsimamia mkandarasi. Ni wazi hivyo hivyo, kazi zote zitafanywa na vijana wa Sogoo. Tutaweka maofisa wawili na kila jioni watanipa ripoti ya maendeleo," alisema.
Comments
No comments Yet
Comment